Ushairi

Zijapo Mali.

Kuna nini wanadamu, siwaelewi kabisa,
Mwachosha nitoa hamu, akilini mwanitesa,
Vurugo vyenu vya sumu, kila siku ni mikasa,
Kwa nini zijapo mali, hamkosi ya kusema.

Hamjui Mungu yupo, mpaji wa kila kitu,
Zake sizo za mikopo, apeana kila mtu,
Kwenye shida yeye yupo, Jalali mjawa utu,
Kwa nini zijapo mali, hamkosi ya kusema.

Nikiwa fukara pia, mara nawaomba sana,
Nashindwa kuvumilia, nguvu na uwezo sina,
Maneno mnonambia, ya chuki na kugombana,
Kwa nini zijapo mali, hamkosi ya kusema.

Hali ile ile ile, ndiyo hasa mnapenda,
Wengine wakose yale, wakwame wanakoenda,
Wasifuzu vilevile, maisha ije waponda,
Kwa nini zijapo mali, hamkosi ya kusema.

Wengine wakimiliki, wamilikaji halali,
Wengine hawana haki, wapatapo si halali,
Wapachikwa jina feki, mambo yasiwe sahali,
Kwa nini zijapo mali, hamkosi ya kusema.

(Malenga ni Toney Francis Ondelo)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close