Lugha na Sarufi
Vipengele Vya Fani Katika Fasihi.
Mambo muhimu tunayohitaji kuzingatia tukiangazia fani ni kama yafuatayo.
- Mtindo-Huu ni utaratibu maalum ambao mtunzi wa kazi wa fasihi amefuata kujenga kazi yake.Hutofautiana katika hali ya mtunzi na mtunzi.
- Wahusika-Huweza kujumuisha watu, wanyama na viumbe vingine hai na hata mizimwi.Huwakilisha tabia maalum katika jamii.
- Mazingira/Mandhari-Hapa ndipo mahali ambapo matukio yote ya fasihi hutendeka.Huweza kuwa mazingira halisi au ya kubuni.
- Matumizi ya lugha-Ni mpangilio wa maneno, tamathali za semi kwa ufundi kulingana na mahitaji ya kazi yao.
- Muundo-Hii ni sura nzima ya kazi ya fasihi.