Ushairi

Ukimya uingiapo.

Popote nizungukapo, siwezi vunja miiko,
Nimeshakula kiapo, wewe ndio langu jiko,
Kwahiyo uondokapo, ninaumia kuliko,
Ukimya uingiapo, kwangu ni masikitiko.

Ukimya utokeapo, kwangu ni mahangaiko,
Ninasubiri ijapo, ujumbe kijungu jiko,
Ninaumia iwapo, nitakosa muitiko,
Ukimya uingiapo, kwangu ni masikitiko.

Hakika utowekapo, napata mfadhaiko,
Ndipo chozi lilengapo, na mwisho mbubujiko,
Na chini lidondokapo, napata mtikisiko,
Ukimya uingiapo, kwangu ni masikitiko.

Kaditama iwe hapo, mwisho wa mtiririko,
Unisamehe endapo, umeona badiriko,
Beti chache usomapo, zifanye zenye mashiko,
Ukimya uingiapo, kwangu ni masikitiko.

(MTUNZI: Abdallah Hanga)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close