Fasihi

Uandishi wa ubunifu.

Unaanzaje kuandika?
Kuna aina mbalimbali za uandishi,ikiwemo wa habari,kiuweledi(kiushawishi)uandishi wa kitaaluma(ikisiri) uandishi wa kubuni.

Uandishi wa kubuni ni uandishi unaotokana na uzoefu wa mwandishi pamoja hisia zake kuhusu jambo fulani.Ni uandishi unaojitokeza katika filamu,riwaya,tamthiliya,ushairi na hadithi fupi.

Wataalamu kama Paul Engle( 1963) anastaajabu kuona watu wanapagawa wanapoandika kazi za kubuni. Semzaba (1997) anasema Sana’a huanza na hisia ambazo kila mtu anazo.Ni hisia zinazomsukuma mtu kutunga.

Unaanzaje kutunga?

Kuna kanuni tano ambazo huongoza katika kutunga japo wengine huongozwa na kanuni tofauti.
1.kufanya utafiti
2.uwe na kumbukumbu
3.kuza stadi yako ya uandishi
4.kuwa mbunifu
5.suka ploti iweze kugusa hisia (kuvutia)

Mchakato
1.unatakiwa kuwa na mradi( shajara) ili uweze kutunza kumbukumbu
2.unatakiwa kuchagua nafsi katika uwasilishaji.Nafsi ya 1,2,3.
3.anza kuunganisha visa na matukio(mpangilio wa kimantiki wa hadithi) mfano ulizaliwa-ukasoma-kuolewa/kuoa-kuzaa nk.unatafuta namna ya kuunganisha inayovuti.
4.kuumba wahusika watakaobeba wahusika mbalimbali na kuwapa majukumu
5.baada ya kuchagua nafsi baada ya kupangilia visa na mikasa na vituko,baada ya kuwaumba wahusika na kuwapa wahusika zao.Anza kuandika

Hitimisho
Ukitaka uwe mwandishi mahiri ni lazima uwe msomaji wa kazi za wenzako.

(Makala haya yameandaliwa na George Mapundo)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close