Tulia Tupendane.
NAKUITA BEBI WANGU, NISIKIYE WE MWANDANI.
UWELEWE HAYA YANGU, UYAWEKE NA KICHWANI.
USIHOFU NA MAJUNGU, WANAYONENA JIRANI.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
WENGI HAWAKUAMINI, KWAMBA MI NITAKUOA.
MOYO UKALA YAMINI, UTAKUJA KUNILEA.
JINA NA KWITA WE HANI, WASIJE KUKUSUMBUA.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
KWA MBALI WAKIKUONA, TAYARI NIMESHA SENDI.
SIYO MAMBO KUNGOJANA, KWA KWELI MIE SIPENDI.
TUMBO WAKISHA LIONA, NI DHAHIRI HAWAPENDI.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
MANENO WATAYALETA, WA KWAMBIE MI SIFAI.
NA MBINU WAKITAFUTA, WANITOWE NA UHAI.
UGONJWA NIKIUPATA, NITABAKI NIKO HOI.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
NIPENDE MAMA MWENZAKO, TUISHI VYEMA DAIMA.
AMINI MIE NI WAKO, SIZIPENDI NA DHULUMA.
NITAJIACHIA KWAKO, TUMUOMBE NA KARIMA.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
MAHASIDI IWAUME, WATUACHE TUSHIBANE.
MIE MWENYEWE KIDUME, SI WA MIRABA MINNE.
UMBALI WAJISUKUME, WAKOGE TENA WACHANE.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
SASA NAKATA SHAURI, ATAZALIWA MWANANGU.
MWISHO WA LANGU SHAIRI, UJUMBE NDIO WA KWANGU.
NITAMUOMBA KAHARI, MKE UKOSE UCHUNGU.
WE TULIA TUPENDANE, WAJINGA WAULIZANE.💞
(MTUNZI:SAID MRUU)