Ngeli za Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili ina ngeli nyingi sana.Baadhi yazo bado yafanyiwa utafiti na wataalam mbalimbali wa lugha ili kuidhinisha matumizi yake.K.m Ngeli ya VI-VI ambayo ina nomino nomino moja tu inayojumuishwa humo yaani vita. Ngeli zinazotumika aghalabu ni kama zifuatazo. Ngeli ya A-WA-Hii ni ngeli ya vitu vilivyo na uhai kama vile wanyama,ndege, binadamu, wadudu n.k.BaadhiContinue reading “Ngeli za Kiswahili.”

Aina za Shamirisho/Yambwa.

Shamirisho ni nomino katika sentensi inayoonyesha/inayoashiria mtendwa/kitendwa na mtendewa/kitendewa.Kuna aina tatu za shamirisho. Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa. Shamirisho Kitondo/Yambiwa/Yambwa Tendewa. Shamirisho Ala/Kitumizi. Shamirisho Kipozi.Hii ni nomino inayoathiriwa na kitenzi katika sentensi kwa njia ya moja kwa moja.K.m Mchezaji alipiga mpira.Shamirisho Kitondo.Hii ni nomino isiyoathirika na kitendo kwa njia ya moja kwa moja.K.mMtoto alimjengea mama nyumba.Shamirisho Ala.HiiContinue reading “Aina za Shamirisho/Yambwa.”

Aina Za Ndege.

Dudumizi/Shundi/Gude/Tipitipi-Huyu ni aina ya ndege asiyejenga kiota. Kanga-Huyu ni kuku wa porini aliye na madoadoa meupe. Kasuku-Ndege aliye na rangi nyingi za kupendeza na hodari wa kuiga. Kigotago-Ndege ambaye hupigapiga mti kwa mdomo ili kupata vidudu. Hondo-Ndege aliye katika jamii moja ya shundishundi aliye na maji ya kunde na hupaza sauti kwa kawaida yake. Chozi-NdegeContinue reading “Aina Za Ndege.”

Aina za Viambishi.

Kuna aina mbalimbali ya viambishi kama ifuatavyo. Viambishi awali-Hivi ni viambishi vinayopachikwa/kuambatanishwa kabla ya mzizi wa kitenzi.K.m a-na-pik-a.a-na ni viambishi awali. Viambishi tamati-Hivi ni viambishi vinayopachikwa/kuambatanishwa baada ya mzizi wa vitenzi.K.m a-na-kul-a.a ni kiambishi tamati. Dhima ya viambishi.Viambishi Awali. Huonyesha nafsi, wakati na idadi.K.m a-na-chek-a.Hapa tunapata nafasi ya tatu, umoja, wakati uliopo,hali ya kuendelea. HuonyeshaContinue reading “Aina za Viambishi.”

Fani za Uandishi/Kisanaa.

Hizi ni mbinu za Kiufundi zitumikazo na mwandishi/msimulizi wa kazi yoyote ya fasihi ambayo humlazimisha msomaji/hadhira kuisoma hadithi nzima ili kuzitambua.Baadhi yazo ni kama vile: Sadfa-Hii ni hali ambapo matukio hutendeka kwa pamoja bila ya kupangwa. Kisengerenyuma-Hapa mwandishi hurejelea matukio yaliyofanyika nyuma.Hivyo humlazimu kubadilika wakati kuyasimulia tena. Kisengerembele-Hapa mwandishi husimulia mambo yatakayotokea siku za halafuContinue reading “Fani za Uandishi/Kisanaa.”

Aina za vihusishi.

Vihusishi ni aina ya maneno yanayoonyesha uhusiano baina/kati ya neno moja na jingine.Kuna aina mbalimbali za vihusishi kulingana na utendakazi wao.Dhima za vihusishi ni kama zifuatazo. Hutumika kuonyesha uhusiano kiwakati.K.m Wanafunzi walienda darasani baada ya kusikiliza hotuba ya mwalimu mkuu. Hutumika kuonyesha uhusiano wa mahali.K.m Walitembea kando ya barabara. Hutumika kuonyesha uhusiano wa umilikaji.K.m WageniContinue reading “Aina za vihusishi.”

Salamu za Kiswahili.

Katika lugha ya Kiswahili kuna jinsi husubahiana na kujuliana hali.Aghalabu hutegemea wakati unapotumika na wahusika kuzingatia kigezo cha umri.Baadhi ya salamu za Kiswahili ni kama zifuatazo. Alamsiki-Hii salamu hutumika usiku wakati mmoja anaaga mwengine.Jawabu ni binuru. Salaam aleikum-Hii ni salamu inayotumika wakati wowote na baina ya mtu yeyote na mwengine.Jawabu ni aleikum salaam. Hujambo-Hii piaContinue reading “Salamu za Kiswahili.”

Aina za viunganishi.

Viunganishi ni aina ya maneno yanayotumika kuunganisha neno moja na jingine, sentensi moja na nyingine au kujaribu kuonyesha uhusiano kati ya dhana mbili au zaidi.Kuna aina mbalimbali za viunganishi kulingana na utendakazi wao katika sentensi. Vya kuonyesha sababu-Mifano ni kama vile madhali, maadamu,kwa minajili ya, kwa kuwa,ili, kwani, kwa vile n.k.K.m Mwanafunzi huyu hakuja shuleniContinue reading “Aina za viunganishi.”

Aina za virai.

Kirai ni kipashio cha kimuundo kinachoundwa kwa neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.Kuna aina mbalimbali za virai kama zifuatazo. Kirai Nomino(KN)-Hiki ni kifungu cha maneno ambacho neno lake kuu ni nomino.K.mVijana kwa wazee walihudhuria mkutano wa jana. Kirai Kitenzi (KT)-Hiki ni kifungu cha maneno ambacho neno lake kuu ni kitenzi.K.mContinue reading “Aina za virai.”

Aina za viwakilishi.

Kiwakilishi ni neno linalotumika/linalosimamia nomino.Katika Kiswahili kuna viwakilishi mbalimbali kama zifuatazo. Viwakilishi vya sifa-Hutumika kwa niaba ya nomino kuonyesha sifa yake.K.m Vitamu vimeliwa. Viwakilishi vya A-Unganifu-Hutumika kwa niaba ya nomino kwa kuonyesha kinachomiliki nomino hiyo.K.m Cha mkufu mwanafu hali. Viwakilishi vya nafsi-Hutumika kwa niaba ya nafsi.Mifano yazo ni mimi, sisi, wewe, nyinyi,yeye,wao.Sisi tulikula tukashiba. ViwakilishiContinue reading “Aina za viwakilishi.”