Nafasi ya Kiswahili Barani Afrika.

*NAFASI* *YA* *KISWAHILI* *KATIKA* *BARA* *LA* *AFRIKA* ! Swali ambalo tunafaa kulijua tunapoangazia suala hili ni, je! Mswahili ni nani?, Kiswahili kilitoka wapi?. Hilo ni suala la kiisimu ambalo pengine nitaligusia kidogo. Kuna maono mbalimbali kuhusu huyu anayeitwa mswahili. Mwandishi wa _periplus_ katika katika usemi wake anadai kuwa: a). Waswahili ni wajuzi wa meli- yaaniContinue reading “Nafasi ya Kiswahili Barani Afrika.”

Dhana Ya Fonetiki.

Fonetiki ni taaluma inayojishughulisha na jinsi sauti yo yote inavyotolewa au inavyopatikana. Hii ni sayansi huru ambayo inatumia nadharia za sayansi halisi kama vile fizikia, uhandisi, baiolojia, nk. na kufaidi matokeo ya kiutafiti ya taaluma hizi. Mathalani, ili mwanafonetiki aelewe jinsi ala za sauti zinavyofanya kazi wakati wa utolewaji wa sauti, atafaidika na maelezo yaContinue reading “Dhana Ya Fonetiki.”

Matumizi Ya Lugha.

Matumizi ya lugha ni namna ambavyo wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa kuzingatia mila, desturi na kaida mbalimbali za jamii inayohusika. Katika mada hii utajifunza mambo ya msingi ya kuzingatia unapotumia lugha. Utaelewa dhana mbalimbali zinazohusishwa na matumizi ya lugha kama vile rejesta, misimu, utatata katika lugha, lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi. MatumiziContinue reading “Matumizi Ya Lugha.”

Dhana Ya Jamii Lugha.

Kwa mujibu wa Mekacha (2011) dhana ya jamii lugha imetafsiriwa kwa mitazamo mbalimbali, hata hivyo wataalamu wengi wanakubaliana na maana ya jumla kuwa jamii lugha ni watumiaji wa lugha wanaoishi katika eneo moja ambao hubainishwa kwa mahusiano yao ya kuendelea kutumia aina fulani ya lugha tofauti na watumiaji wengine wa lugha hiyohiyo. Licha ya fasiliContinue reading “Dhana Ya Jamii Lugha.”

NAFASI YA KISWAHILI

NAFASI YA KISWAHILI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.UTANGULIZIKiswahili kimeibuka kuwa la muhimu katika tamaduni nyingi zilizopo Afrika Mashariki. Wakati wa enzi za ukoloni katika Afrika Mashariki,haja ya kuwepo kwa lugha moja itakayotumika hususan katika elimu katika nchi zote za makoloni ya mwingereza wakati ule,yaani Tanganyika,Kenya,Uganda ilijitokeza. Isitoshe, baada ya nchi nyingi za Afrika Mashariki kupataContinue reading “NAFASI YA KISWAHILI”

NGELI YA KI-VI.

Hii ngeli husheheni maneno mengi ya lugha ya Kiswahili.Baadhi yazo ni yale yaliyowekwa katika udogo kwa kupachikwa kiambishi Ki mwanzoni mwa kila neno.Mifano ni kama Kiguo,kijishamba,kijitu,kijipanya n.kMifano ya maneno mengine yanayopatikana katika ngeli hii ni kama vile kiatu,kikombe, kinyonyi, kibarua, kivumishi, kitengo n.k Muundo wa ngeli ya A-WA Kwa kuna maneno yanayoanza na kiambishi‘Ki’ naContinue reading “NGELI YA KI-VI.”

Mashairi Ya Tarbia.

TAKUENZI MOYONI. Moyoni uwe peke yako, wewe kipenzi cha moyo. Nakupenda pekeako, hakuna mwingine huyo.Ila nasema ni kwako, wengine ni sagamoyo.Pendo letu limoyoni,takuenzi aushini. Kwako mimi sibanduki,chaguo langu la moyo.Kwingine mimi sitaki,ni wewe kipenzi changu.Kama asali ya nyuki, napenda uwe wa kwangu.Pendo letu limoyoni, takuenzi aushini. Hatimaye lije zaa, matunda mazuri pendo.Mahari tapelekea, yenye mazuriContinue reading “Mashairi Ya Tarbia.”

Matumizi Ya Ki.

Kiambishi ‘Ki’ kinatumika kwa njia mbalimbali kama zifuatazo. Ki ya Masharti.K.m Ukisoma kwa bidii utafaulu maishani. Ki ya kuwakilisha Ngeli ya KI-VI.K.m Kikombe hiki ni safi sana. Ki ya udogo.K.m Kiguo hiki kimechafuka. Ki ya mfanano.K.m Mtoto yule amelala kifudifudi. Ki ya kuonyesha kitendo kinachofanyika kwa wakati mmoja.K.m Mama anakula akiona runinga. Ki ya kukanushaContinue reading “Matumizi Ya Ki.”

Aina za bahari ya mashairi.

Kuna aina mbalimbali za mashairi kwa kuzingatia kigezo cha bahari. Sakarani-Hili ni shairi lenye bahari zaidi ya moja. Ukara-Hili ambalo vina vya kipande kimoja hubadilika kutoka ubeti moja hadi mwingine ilhali vina vyaupande mmoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Ukaraguni-Hili ni shairi ambalo vina vya kati na vile vya mwisho hubadilika kutoka ubeti mmojaContinue reading “Aina za bahari ya mashairi.”

Matumizi Ya Kiambishi Na.

Kiambishi ‘na’ hutumika kwa njia tofauti katika sentensi ili kuonyesha maana mbalimbali kama ifuatavyo: Hutumika kuonyesha dhana ya wakati uliopo.K.m Mama anapika chakula. Hutumika kama kiunganishi katika sentensi.K.m Neema na Fadhili wanacheza mpira. Hutumika kuonyesha dhana ya umilikaji.K.m Juma ana kalamu nzuri. Hutumika kuonyesha mtendaji wa kitendo.K.m Mpira huo ulipigwa na Mwadime. Hutumika kuonyesha kauliContinue reading “Matumizi Ya Kiambishi Na.”