Ushairi

Suti meniteka moyo.

Suti meniteka moyo, kwa huu urembo wako, Mate yanitoka mbiyo, nina hamu kuwa wako, Pesa nayo yote hayo, sifanye n’siwe wako, Jaribu kushusha bei, elfu mbili naweza.

Weye suti una nini, tangu utoke Ulaya, Metoka ughaibuni, hadi nchi ya umbeya, Maringo yako ya nini, au tai yavutiya, Jaribu kushusha bei, elfu mbili naweza.

Naomba yako huruma, mitaani nikuvae, Nikialikwa na uma, shereheni nikuvae, Wasinilishe sukuma, birihani wanifae, Jaribu kushusha bei, elfu mbili naweza.

Nitaenda mialiko, mialiko mbalimbali, Makongamano niliko, uchina hata na Mali, Kwenye ndege takuweko, kufundisha Kiswahili, Jaribu kushusha bei, elfu mbili naweza.

Nimeshapanda tayari, meongeza mia mbili, Hilo eneo hatari, ipunguze mara mbili, Hino bei si hatari, takuongeza Jalali, Jaribu kushusha bei, elfu mbili naweza. Sijaudhika ni sawa, ni sawa kwa kuniruka, Najua nitajaliwa, siku yangu itafika, Nitavaa maridhawa, nisitengwe Afirika, Jaribu kushusha bei, elfumbili naweza.

(Malenga ni Toney Francis Ondelo)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close