Sinibague kamwe.
SINIBAGUE KAMWE
Sinibague silani,maana wewe tajiri
Nihurumie jamani,hali yako sisitiri
Sinione kwa utani,nipee haki dhahiri
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
Nipeni nafasi wana,niwaelezee hima
Kuona juzi na Jana,kutibuka yao jama
Wenyewe wakapigana,tabia zile za nyuma
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
Sinayo hata elimu,wewe unazo shahada
Heshima kwangu muhimu,nipe haki ewe Dada
Sinibague kwa zamu,akilini sina shida
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
Kabila sikuchagua,Masikini sikupenda
Mbonaa kunibagua,mabaya nayo kutenda
Wazidi kunikagua,lako haja kunikanda
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
Ngozii yangu nyeusi,kanipa ewe rabana
Mbona bwana wanitusi,na kuibadili jina
Kuniitaa mjusi,kwa vigezo twafanana
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
Shairi natamatisha,ukurasa kuufunga
Ujumbe umewatosha,Mmeipataa kinga
Ubaguzi unatisha,nasitakoma kutunga
Usinibague kamwe,nipe heshima nilivyo
(Malenga Mhanguzi)
Kazi Safi guru