Mabadiliko ya tabia-nchi

Siku ya mazingira duniani.

[wpvideo 9QvPg2Z0 data-temp-aztec-id=”c7bc5b82-c0ad-49f9-b60a-715a603afa06″]Siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila mwaka juni 7 ili kuangazia hatua ambayo jamii ya kimataifa imepiga kutunza mazingira.Chakula tunayokula,maji tunayoyanywa,hewa tunayopumua na mengine mengi yanatoka kwenye mandhari yetu.Mwaka huu wa 2020 tunaangazia hatua madhubuti dhidi ya uchafuzi wa mazingira kwani mandhari yetu yashaanza kutupa ujumbe kuwa tusipohadhari tutaangamia.Ili kujilinda lazima kwa vyovyote vile tulinde mazingira.Huu ndio wakati mwafaka kuamka kutoka usingizi wa pono na kupaza sauti kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.Mwaka huu kauli mbiu ni binadamu na dunia.Kama njia moja ya kuhakikisha mafanikio ya kutunza,nchi nyingi duniani zimeafikiana kutupilia mbali matumizi ya gesi chafu kufikia mwaka 2050.Kampuni nyingi tu zimekubali hii hatua.Ikumbukwe maadhimisho haya yanakuja wakati ambapo duniani unakabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close