Lugha na Sarufi

Salamu za Kiswahili.

Katika lugha ya Kiswahili kuna jinsi husubahiana na kujuliana hali.Aghalabu hutegemea wakati unapotumika na wahusika kuzingatia kigezo cha umri.Baadhi ya salamu za Kiswahili ni kama zifuatazo.

  1. Alamsiki-Hii salamu hutumika usiku wakati mmoja anaaga mwengine.Jawabu ni binuru.
  2. Salaam aleikum-Hii ni salamu inayotumika wakati wowote na baina ya mtu yeyote na mwengine.Jawabu ni aleikum salaam.
  3. Hujambo-Hii pia hutumika wakati wowote na baina ya mtu yeyote na mwengine.Jawabu ni sijambo.
  4. Cheichei-Hii hutumika mara nyingi na watu wenye umri uliokaribiana (mariika). Hutumika wakati wowote.Jawabu ni ewaa.
  5. Sabalkheri-Hutumika baina ya mtu mkubwa na mtu mwingine mkubwa majira ya asubuhi.Jawabu ni alkheri.
  6. Masalkheri-Hutumika pia baina ya watu wakubwa majira ya jioni.Jawabu ni alkheri.
  7. Shikamoo-Hii ni salamu itumikayo baina ya mtu mdogo na mtu mkubwa kwa umri.Hutumika wakati mtu amekutana mwingine kwa mara ya kwanza siku hiyo.Jawabu ni marahaba.
  8. Habari-Hii hutumika wakati wowote.Jawabu ni nzuri/njema.
Tags
Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close