Ushairi
Pakacha.
Mie mwenyewe niliacha Wala hakuniwata
Nitembelee pancha Akhii wacha utata
Ilo lingali pakacha lawaka bila mafuta
Umeibeba pakacha kesha waombe mvua inyeshe
Si la kuyaficha mambo wala kuwa na sitara
Sijazoea nichambo maneno yanayo kera
Simlaji wa makombo umezoea kafara
Umeibeba pakacha kesha waombe mvua inyeshe
Halisitiri kwa jua wala ijapo mvua
Nahilo nimelisua mwilini nikalivua
Wajisifia na bua haya machache chukua
Umeibeba pakacha kesha waombe mvua inyeshe
(Malenga ni Abuuabdillah)