Matumizi Ya ‘Kwa’.

‘Kwa’ hutumika kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo:

 1. Kuonyesha dhana ya pamoja na .K.m Wasichana kwa wavulana walihudhuria mkutano.
 2. Kuonyesha kifaa au chombo kilichotumika.K.m Fundi alichota changarawe kwa sepetu.
 3. Kuonyesha akisami.K.m Yeye alizoa alama tisa kwa kumi.
 4. Kuonyesha uhusiano kati ya mtu/watu na mahali.K.m Nitaenda kwa mwalimu kumtembelea.
 5. ‘Kwa’ ya A-unganifu.K.m Kuimba kwa wanafunzi kuwafurahisha walimu.
 6. Kuonyesha dhana ya kielezi.K.m Tulimkaribisha mgeni kwa mkono mkunjufu.
 7. ‘Kwa’ ya Kiulizi.K.m Kwa nini umechelewa kuja darasani?
 8. Kwa kumiliki ya nafasi ya kwanza umoja katika ngeli ya KU-KU.K.m Kucheza kwangu kulifurahisha wengi.

Matumizi Ya ‘Kwa’.

‘Kwa’ hutumika kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo:

 1. Kuonyesha dhana ya pamoja na .K.m Wasichana kwa wavulana walihudhuria mkutano.
 2. Kuonyesha kifaa au chombo kilichotumika.K.m Fundi alichota changarawe kwa sepetu.
 3. Kuonyesha akisami.K.m Yeye alizoa alama tisa kwa kumi.
 4. Kuonyesha uhusiano kati ya mtu/watu na mahali.K.m Nitaenda kwa mwalimu kumtembelea.
 5. ‘Kwa’ ya A-unganifu.K.m Kuimba kwa wanafunzi kuwafurahisha walimu.
 6. Kuonyesha dhana ya kielezi.K.m Tulimkaribisha mgeni kwa mkono mkunjufu.
 7. ‘Kwa’ ya Kiulizi.K.m Kwa nini umechelewa kuja darasani?
 8. Kwa kumiliki ya nafasi ya kwanza umoja katika ngeli ya KU-KU.K.m Kucheza kwangu kulifurahisha wengi.

Alama Za Uakifishaji.

Kituo/Nukta.(.)Hutumika kwa njia zifuatazo:

 1. Hutumika mwishoni mwa sentensi.K.m Mwanafunzi ameshindwa kusoma vema.
 2. Hutumika katika uandishi wa tarehe.K.m 21.03.1998
 3. Hutumika katika uandishi wa vifupisho.K.m Daktari-Dkt.
 4. Hutumika mwishoni mwa orodha ya vitu.K.m Mama alinunua maembe, machungwa,nanasi na ndizi.

Koma/Kipumuo/mkato. (,)

 1. Hutumika kutenganisha vitu vilivyoorodheshwa.K.m Mwanafunzi amenunua kitabu,kalamu na sare ya shule.
 2. Hutumika kuonyesha pumziko kidogo katika sentensi.K.m Tulipofika hotelini,mama aliagiza aletewe chakula.

Nuktapacha (:)

 1. Hutumika kutenganisha dakika na sekunde.K.m 1.28:29
 2. Hutumika kutenganisha kichwa/mada kuu na ndogo.K.m Sarufi ya Kiswahili:Ngeli za Kiswahili.
 3. Hutumika kutenganisha vitu vilivyotajwa katika orodha. K.m Kule sokoni tulinunua vitu vifuatavyo:mboga,chumvi, nyanya na kitunguu.
 4. Hutumika kutenganisha sentensi mbili zenye uzito sawa na zilizokamilika.K.m Baba analima:mama anafua.

Mkwaju/Mtoi.(/)

 1. Hutumika badala ya neno ama/au.K.m Baba/mama.
 2. Hutumika kubainisha matamshi.K.m /M’ti /
 3. Hutumika badala ya neno ‘kwa’.

Nuktamkato.(;)

 1. Hutumika kutenganisha vitu vilivyopo katika sentensi.K.m Ili nifike Nairobi nilipita miji kama;Kakamega,Kisumu,NaKuru na Kiambu.
 2. Hutumika kutenganisha dhana mbili za sentensi ambatani.K.m Baba alikuja nyumbani saa mbili; alikuwa ameenda kazini.

(Kamusi kuu ya Kiswahili, Longhorn Publishers,2016).

Sifa Za Mhakiki.

Mhakiki huwa na sifa zifuatazo:

 1. Anatakiwa asikuwe mpondaji wa kazi ya watu wengine; asichukue au kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila ya kuzingatia ukweli wa kazi hiyo.
 2. Mhakiki anastahiki awe amesoma kazi mbalimbali za fasihi na sio tu ile anayoifanyia uhakiki ili awe na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.
 3. Mhakiki anatakiwa asome tahakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi hata nje ya jamii ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki.
 4. Mhakiki anastahiki aelewe historia na siasa ya jamii inayohusika.Hili litamwezesha kuelewa matatizo ya jamii hiyo.
 5. Mhakiki anatakiwa ajue historia na mazingira yaliyomkuza mwandishi.

Aina za vielezi.

Kielezi ni neno linafafanua/linapambanua kitendo/kitenzi.Hueleza kitendo kilifanyika vipi,wapi,lini na mara ngapi.

Kutokana na maelezo haya tunapata aina zifuatazo za vielezi:

 1. Vielezi vya wakati/njeo k.m Mgeni atawasili asubuhi.’Asubuhi’ ni kielezi cha wakati.
 2. Vielezi vya mahali k.m Walimu wale wanaenda shuleni.’Shuleni’ ni kielezi cha mahali.Aghalabu vielezi hivi hutamatika kwa kiambishi ‘ni’.
 3. Vielezi vya namna/jinsi k.m Tulitembea harakaharaka tukienda sokoni.’Harakaharaka’ ni kielezi cha namna.
 4. Vielezi vya idadi/kiasi k.m Mgeni yule huwa anatembelea mara kwa mara.’Mara kwa mara’ ni kielezi cha idadi.

Tanbihi:Kila aina ya kielezi huweza kuainishwa katika vikundi vingine vidogo.

Aina za vivumishi.

Kivumishi ni neno linalofafanua nomino, kivumishi kingine au hata kiwakilishi.

 • Kuna aina nyingi za vivumishi kama vile:
 • Kivumishi cha pekee k.v -enye,-enyewe,-ingine-,-ote,-o-ote.
 • Kivumishi cha idadi-Hapa kuna kivumishi cha idadi kamili k.v moja,mbili,tatu n.k na kivumishi cha idadi isiyodhihirika k.v -ingi,-chache.
 • Kivumishi cha A-unganifu k.v cha,wa,la n.kVivumishi viulizi k.vgani,-pi,-ngapi,-api n.k
 • Vivumishi vya sifa k.v -eusi,-ekundu,-fupi,-refu n.kVivumishi viashiria/vionyeshi k.v huyu,huyo,yule n.k
 • Vivumishi vimilikishi k.v -angu,-etu,-ao n.kVivumishi visisitizi k.v yuyu huyu,yuyo huyo n.k
 • Vivumishi viradidi k.v huyu huyu,huyo huyo,yule yule n.k
 • Vivumishi virejeshi k.v amba-, O-rejeshi n.k
 • Shairi la Arudhi.

  Safiri Salama Rais Mstaafu Moi.

  Huzuni ‘nayo Moyoni, sisi Kama wanakenya
  Alfajiri huzuni,baba Moi kafariki
  Tutakutia wazoni, Ni mengi uliyatenda
  Rais mstaafu Moi,safiri salama uko

  Hatuna pia matata,kila kitu ni bayana
  Hulikataa ka’kata,kutenganisha wakenya
  Wanakenya tulidata,Moi kaboresha kenya
  Rais mstaafu Moi, Safiri Salama uko

  Mashule uliyajenga, mazahanati tunayo
  Wakenya hata makanga ,maziwa nyayo wakanywa
  Barabara alijenga,maendeleo kafanya
  Raise mstaafu Moi, Safiri Salama
  Uko
  (bosiredaniel12@gmail.com)

  Shairi La Tarbia.

  Kalamu ni hii yangu, hisia zangu nitoe
  Kiniumacho wezangu, Mimi nimwambiee
  Siwachoshi Somo zangu,nasukumwa nimwambie
  Nipendaye hanipendi,anipendaye sipendi

  Wenzangu naomba jua,Nani mapenzi kaumba
  Kama Ni Mola kaumba,Semeni nijue pia
  Naumia tena sana,maanake nampenda
  Nipendaye hanipendi, anipendaye sipendi

  Mrembo nimpendaye,jinake ngumu kusema
  Nilidhani baadaye,mahari mie ningetoa
  Wajomba na wazaziye,mahari wangepokea
  Nipendaye hanipendi, anipendaye sipendi

  Moyoni nasononeka, Mimi mpenda shairi
  Sitaki ‘zidi andika,yanitoka tiritiri!
  Ningezidi kuandika,mtima ‘ngu waghairi
  Nipendaye hanipendi,anipendaye sipendi

  (Malenga: bosiredaniel12@gmail.com)

  Dhana Ya Sintaksia.

  Hii ni taaluma inayoshughulikia uchunguzi wa mpangilio na uhusiano wa vipashio vya sentensi.

  Katika kiwango hiki tunachunguza jinsi ambavyo maneno ya kategoria mbalimbali zinazokubalika na zenye maana.

  Maneno ya kategoria mbalimbali ni kama vile nomino,vitenzi,viwakilishi,vivumishi,vielezi n.k

  Maneno haya hayafuatani kiholela;huungana kwa kufuata sheria za kiisimu ili kujenga sentensi zinazokubalika na zenye maana katika lugha.

  Nomino na vivumishi huweza kutumika kwa pamoja.Baadhi ya vivumishi huweza kutoa kabla ya nomino.K.m Yule mwanafunzi anasoma kwa bidii.

  Vielezi huweza kufuata/kufuatana na vivumishi k.m Mfupi tena sana.

  Kipashio cha kimsingi katika taaluma hii ni sentensi.

  Aidha, taaluma hii huchunguza kategoria za maneno kulingana na utendakazi wake katika sentensi.Kategoria hizi hutumika katika uchambuzi wa sentensi za lugha.

  Katika uchambuzi wa sentensi tunatumia taratibu mbalimbali za kisintaksia.Katika sentensi tunapata kundi nomino na kundi tenzi.Katika kundi nomino tunapata virai na vishazi mbalimbali.

  Tunapata dhana mbili ambazo ni kiima na kiarifa katika kuigawa sentensi.Sehemu ya kiima huwakilisha kutenda/mtenda k.m Neema amefariki.Isitoshe hubeba kikundi cha nomino k.m Wanafunzi wawili wasichana kwa wavulana.

  Kiima pia hubeba tungo tegemezi.K.m Mgeni mrefu aliyetembelea jana ataondoka kesho.’mgeni aliyetembelea jana’ ndiyo tungo tegemezi.

  Katika taaluma hii,kuna maneno yanayotumiwa pamoja kwa maana pia pana mengine yasiyoweza kutokea pamoja.K.v N+N,T+V,N+V,E+E n.k.

  Katika taaluma hii pia tunapata kuelewa aina za sentensi.K.v Sentensi sahili, sentensi ambatano na sentensi changamano.

  Dhima ya mhakiki.

  • Kuchambua na kuweka wazi funzo linalojitokeza katik kazi ya fasihi.
  • Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
  • Kutafuta na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
  • Kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi kwa kuzifanyia haki.
  • Kumwelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya mhakiki.
  • Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi.
  • Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi za fasihi.                                          
  %d bloggers like this: