Skip to content

Shairi la Maringo ni ya nini.

MARINGO NI YA NINI? Una damu mishipani, nyekundu kama ya kwangu,Kuishi u duniani, huishi kwenye mawingu,Uyaalayo nadhani, ndo tofauti na yangu,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Unywapo chai maziwa, kwangu nile mkandaa,Sharubati unapewa, nionapo nabung’aa,Japo hapa napagawa, kila siku ni dagaa,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Mavazi unovalia, yametolewa Japani,Yanakushika sawia, siyo kama yangu duni,Matumbani kiingia, bei yangu ishirini,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Yangu duni hudumu, ila yote huzeeka,Yachanikapo haramu, yatupwa kwenye vichaka,Mwenzio hana hamu, zote za deki hakika,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Ulivyonunua gari, hatupumui wenziyo,Mambo kwetu… Read more Shairi la Maringo ni ya nini.

Umuhimu wa Kiswahili.

Kitaifa: Katika kiwango cha kitaifa lugha ya Kiswahili kina majukumu yafuatayo:  Ni chombo cha mawasiliano katika kiwango cha kitaifa, Kikanda na kimataifa kama ilivyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika (UA).  Ni kitambulisho muhimu cha utaifa na uzalendo wetu.  Ni kitambulisho cha watu wa Afrika Mashariki. Kiswahili ni lugha ya taifa na vilevile lugha rasmi nchini Kenya na Tanzania.  Hutumika katika uandishi na uchapishaji. Vitabu vingi vimeaandikwa au kutafsiriwa kwa Kiswahili, kwa mfano Biblia Takatifu, Daftari la Isimujamii.  Ni kigezo cha kuchujia… Read more Umuhimu wa Kiswahili.