Skip to content

Ushairi.

Huu ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum fasaha na yenye muwala kwa lugha ya mkato,sitiari, picha au ishara katika maandishi, usemi au mahadhi ya wimbo ili kueleza tukio au mawazo. Vitu vivanyounda ushairi katika kiswahili ni kama yafuatayo: 1.Takriri-hii ni mbinu ya kurudia jambo kwa madhumuni fulani.Vina na urari wa mizani ni aina ya takriri.Aidha, mshairi anaweza kurudia maneno au silabi fulani kwa dhamira maalum. 2.Taswira-hii ni mbinu ya kuunda picha ya jambo katika fikra ya msomaji/msikilizaji au utungo wenyewe. 3.Tamathali za semi-hapa ndipo tunapata mbinu mbali za lugha zinazoipamba… Read more Ushairi.

Sifa kuu Bainifu za Lugha za Wanadamu.

Sifa zinazotofautisha lugha ya mwanadamu na mfumo wa mawasiliano wa wanyama ni:Unasifu,utabaka,uhamisho na uzalishaji. Unasibu katika lugha ya mwanadamu ni ile hali ambapo sauti fulani zinawakilisha maana fulani katika jamii.Hata zile sauti zinazoingiza mlio wa Sauti nazo pia hukaribia tu ile sauti halisi inayowakilisha (onomatopea). Mengi ya maneno ni sehemu tu ya sauti inayotumika kama ishara inayowakilisha maana ya yale yaliyokusudiwa.Muundo sarufi wa lugha vilevile ni wa kinasibu kwani hakuna muundo wa aina moja mfano wa kirai au kishazi ambao kila lugha hauna budi kuufuata. Utabaka ni ile hali ya… Read more Sifa kuu Bainifu za Lugha za Wanadamu.

Misamiati inayochipuka

1.Generator-kangavuke 2.Greenhouse-Kivungulio 3.Facebook-kitandazi 4.Napiergrass-mabingobingu 5.What’s Up-kunani 6.Herbivores-chelemea 6.Carnivores-mlawangi 7.DNA-msimbojeni 8.Marching-Mwendo-sanjari 9.Icecream-Barafumalai 9.Topcream-utando wa malai 10.Powersaw-msumeno-oto 11.Money laundering-Utakatishaji wa fedha 12.Missed call-simu futu 13.Eardrum-Komangu 14.Intensive care unit-Sadaruki 15.Toothpick-kichokonoa

Tafsiri Za Maneno Katika Kiswahili.

1.Generator-Kangavuke 2.Greenhouse-Kivungulio 3.Facebook-Kitandazi 4.Napiergrass-Mabingobingu 5.What’s Up-Kunani 6.Herbivores-Chelemea 6.Carnivores-Mlawangi 7.DNA-Msimbojeni 8.Marching-Mwendo-sanjari 9.Icecream-Barafumalai 9.Topcream-Utando wa malai 10.Powersaw-Msumeno-oto 11.Flashdisk-Kifyonzi/kinyonyi. 12.Winning goal-Dungu. 13.Internship-Mafunzo ya nyanjani. 14.Commentator-Mrasili. 15.Chlorophyll-Umbijani. 16.Keyboard-Kicharazio. 17.Password-Nywila. 18.Chips-Vibanzi. 19.Scanner-Mdaki. 20.Floppy disk-Diski tepetevu… Read more Tafsiri Za Maneno Katika Kiswahili.

Fonetiki.

Hichi ni kiwango cha lugha kinachoshughulikia sauti za lugha ya mwanadamu kwa ujumla. Taaluma hii kuchunguza namna sauti anuwai ama za irabu au konsonanti hutamkwa kinywani mwa mwanadamu. Katika fonetiki, mwanaisimu huchunguza viungo vinayoshiriki katika utamkaji wa sauti yaani foni.Hujibu maswali yafuatayo: 1.Sauti za lugha ya mwanadamu ni ngapi na ni zipi?Sauti hizo ni nyingi na kuna nyingine ambazo hazijatafitiwa. 2.Sauti za lugha ya mwanadamu hutamkwaje na wapi? Kila mojawapo ya sauti hizo hutamkiwa mahali pake na kwa namna ya kipekee. 3.Foni za lugha ya mwanadamu zinasheheni sifa gani.Mwanaisimu anapochunguza… Read more Fonetiki.