Mhakiki ni nani?

Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa maandishi ya kisanaa hasa yale ya kifasihi.

Mhakiki ni bingwa wa kusoma na kuchambua maudhui yaliyomo katika fasihi.

Yeye hujihusisha na maandishi ya waandishi asilia na kuangalia ni kwa jinsi gani mwandishi anawakilisha hali halisi katika jamii.

Yeye hushughulikia uwanja wa fasihi simulizi na fasihi andishi.

Uendelezaji Wa Fasihi Simulizi Kupitia Katika Karne Ya 21.

Licha ya kuwa fasihi simulizi imekumbwa na changamoto si haba,kuna hatua ambazo zimepigwa kupitia kwa njia zifuatazo.

1.Hadithi zingali zinatambwa katika jamii fulani hasa vijijini.

2.Vipindi vya utegaji na uteguaji wa vitendawili katika redio,runinga na hata kwenye mitandao ya kijamii.

3.Bado kuna michezo ya kuigiza kwenye redio na runinga.K.m Maria-citizen tv.

4.Miviga kama vile mazishi,harusi,Jando n.k ambazo bado tunazishuhudia zinaendeleza utanzu huu.

5.Uchezaji ngoma hasa za kienyeji k.v kirumbizi katika dhifa tofauti k.m za kisiasa.

6.Aidha katika tamasha za muziki, wanafunzi wanapata fursa ya kughani mashairi.

(Fani ya Fasihi Simulizi kwa shule za Upili, Assumpta.K.Matei,2010)

Uendelezaji Wa Fasihi Simulizi Kupitia Katika Karne Ya 21.

Licha ya kuwa fasihi simulizi imekumbwa na changamoto si haba,kuna hatua ambazo zimepigwa kupitia kwa njia zifuatazo.

1.Hadithi zingali zinatambwa katika jamii fulani hasa vijijini.

2.Vipindi vya utegaji na uteguaji wa vitendawili katika redio,runinga na hata kwenye mitandao ya kijamii.

3.Bado kuna michezo ya kuigiza kwenye redio na runinga.K.m Maria-citizen tv.

4.Miviga kama vile mazishi,harusi,Jando n.k ambazo bado tunazishuhudia zinaendeleza utanzu huu.

5.Uchezaji ngoma hasa za kienyeji k.v kirumbizi katika dhifa tofauti k.m za kisiasa.

6.Aidha katika tamasha za muziki, wanafunzi wanapata fursa ya kughani mashairi.

(Fani ya Fasihi Simulizi kwa shule za Upili, Assumpta.K.Matei,2010)

Fani Za Lugha Katika Fasihi.

Fani ni jinsi mambo yanavyosemwa katika fasihi.Yaani ni kipengele katika uwanja wa fasihi kinachojihusisha na umbo la nje la fasihi.Fani za lugha katika fasihi ni kama zifuatazo:

1.Takriri-Hii ni mbinu ya kurudiarudia sauti,silabi,neno au maneno kwa nia ya kusisitiza jambo fulani.K.m Awali ni awali hakuna awali mbovu.Neno ‘awali’ limerudiwa.

2.Taswira-Hii ni picha ya fikra zinazojengeka akilini mwa mtu baada ya kusoma, kusikia ama kushuhudia jambo fulani.

3.Udamisi/Chuku-Hii ni mbinu ya kukipa kitu sifa zaidi ya kiwango kinachokipasa kupewa.

4.Tashihisi-pia hujulikana kama uhaishaji.Hapa kitu hupewa sifa/uwezo za kitu kilicho hai k.v binadamu.k.m Nilitamani ardhi inimeze siku hiyo!

4.Balagha-Haya maswali yasiyohitaji jawabu na huwa na lengo la kumfikirisha mtu.

5.Kinaya-hii ni hali ambapo mambo yanatendeka kinyume na matarajio.

6.Ishara/Taashira-hii ni hali ya kitu fulani kuashiria kingine.

7.Tanakuzi-mbinu hii hutumika pale ambapo kauli/maneno yanapingana.

8.Kejeli/stihizai-hii ni mbinu ya kufanyia mtu utani/mzaha kwa madhumuni ya kupinga tabia zisizofaa.

9.Tashbihi/Tashbiha-Hii ni usemi wa mlinganisho au ufananisho wa vitu viwili kwa kutumia maneno kama vile kama, mithili ya, mfano wa,tamthili ya n.k.K.m Yeye ni mrefu kama mlingoti.

10.Sitiari-Hii ni kinyume cha tashbihi.Hapa vitu hulinganishwa bila kutumia maneno ya kulinganisha.K.m Baba ni simba.Hii ina maana baba ni mkali kama simba.

11.Tanakali za sauti-Hapa sauti za vitendo au vitu huigwa.K.m Alianguka chini pu!

12.Methali-Hizi ni semi za kimapokeo ambao hutoa kauli za kuonya, kuelimisha au kupongeza kwa njia ya busara.K.m Hasira hasara.

(Fani ya Fasihi simulizi kwa shule za upili,Assumpta .K. Mateo,Kamusi kuu ya Kiswahili, Longhorn publishers)

Aina za sentensi za Kiswahili.

Sentensi huainishwa kuzingatia vigezo mbalimbali.Hapa tutaangazia aina za sentensi kimuundo kama ifuatavyo:

1.Sentensi sahili-Hii ndio sentensi ya kimsingi katika lugha na huwa na kiima na kiarifa kimoja tu.Aidha,husheheni wazo/dhana moja tu.K.m Mtoto anasoma.

2.Sentensi ambatano/ambatani-Hii ni mjumuiko wa vishazi huru viwili.Hapa kuna muungano wa sentensi mbili zenye uzito sawa.Sifa zake ni: huwa na vishazi viwili au zaidi na kuna matumizi ya viunganishi mbalimbali k.v japokuwa,ilhali,minghairi ya,kwa sababu n.k.K.m Muziki unaimba huku watoto wakicheza.

3.Sentensi changamano/changamani-Hii ni sentensi inayosheheni vishazi viwili yaani kishazi huru na tegemezi.Kishazi huru hujisimamia kama sentensi kamili (sentensi sahili) ilhali kishazi tegemezi ni tungo isiyo kamili yaani inategemea kishazi huru ili ikamilike.Kishazi tegemezi pia hutoa habari zaidi kuhusu kishazi huru.K.m Nguo ambazo zilioshwa leo asubihi zitakauka leo jioni.Aghalabu aina ya sentensi hii huwa na matumizi ya amba- rejeshi au O- rejeshi.

Ngeli ya A-WA na muundo wake.

Ngeli hii hutumika sana kwa vitu vilivyo hai mathalan wadudu,wanyama,ndege, binadamu n.k

Ikumbukwe kuwa tunapozungumzia binadamu,tusisahau kuwa atapoaga hivyo kuwa maiti bado anahitaji heshima zake hivyo maiti apo katika hii ngeli.Ni makosa ya kisarifu kusema ‘Maiti ilizikwa’.Ila tunasema ‘Maiti alizikwa.’

Muundo ya ngeli hii inadhihirika kama ifuatavyo:

1.MU k.v katika neno ‘Muumba.’

2.M k.v katika neno ‘Mtu’

3.MW k.v katika neno ‘Mwanafunzi’.

4.KI k.v katika neno ‘kiroboto’

Miundo Ya Silabi Za Kiswahili.

Kuna miundo mbalimbali za silabi za kama ifuatavyo.

1.Silabi za Irabu pekee k.v katika maneno kama vile oa na ua.

2.Silabi za K+I-Hapa ndipo maneno mengi ya Kiswahili yanapatikana.Maneno huwa na silabi moja, mbili au zaidi.Mifano ipo katika maneno kama vile mama,baba n.k

3.Silabi za K+K+I-Konsonanti za mwanzo katika muundo huu huwa na vitamkwa vya ving’ong’o/nazali.Mifano ya maneno ni kama ndevu,Mbacha n.k

4.Silabi za K+k+I-Hapa konsonanti huwa mwanzo kisha kufuatiwa na kiyeyusho na kumalizika kwa irabu.Mifano ya maneno yenye silabi za muundo huu ni kama vile mbwa,mwadhama n.k

5.Silabi za K+K+K+I-Muundo huu hushamiri katika maneno yaliyoswahilishwa/kukopwa kutoka lugha za Kigeni.Mifano ya maneno ni kama vile Skrubu n.k

6.Silabi za K+I+K-Maneno yaliyo na muundo huu ni yale ya kibantu au yaliyokopwa.Silabi funge hushamiri hapa sana.Mifano ya maneno ni kama vile labda, teknolojia n.k

(K inasimamia konsonanti,k inasimamia kiyeyusho (/w/ na /y/),I inasimamia irabu.

Aina Za Silabi.

Silabi ni mpigo mmoja wa sauti.Kuna aina mbili kuu za silabi katika lugha ya Kiswahili.

Aina ya kwanza huitwa silabi huru/wazi.Silabi hii mara nyingi huishia kwa irabu.Sauti za silabi hii husikika kwa nguvu.Mifano ya maneno yenye silabi hii ni kama vile lala,Ndaki, sebule n.k

Ya pili inajulikana kama silabi funge.Hii silabi nayo hishia kwa konsonanti.Mifano ya maneno yenye silabi hii ni maneno yaliyokopwa mathalani labda, alhamisi n.k.

Tofauti kati ya Fonolojia na Fonetiki.

Licha ya kwamba taaluma ya fonolojia na fonetiki hukaribiana sana, kutegemeana na kukamilishana kwa kuwa zote huchunguza sauti, kuna tofauti kadhaa kama zifuatazo.

1.Uchunguzi wa kifonolojia huzingatia mfumo maalum wenye utaratibu fulani ilhali uchambuzi wa kifonetiki.

2.Uchambuzi wa kifonolojia huzionyesha zile sifa bainifu katika lugha mahususi.Kwa upande mwingine taaluma ya fonetiki huorodhesha sauti zote na kutoa ufafanuzi kiumakinifu zinazoonesha tofauti zote za kifonetiki katika foni.

3.Fonolojia huwa nyingi kama idadi ya lugha zilizopo duniani kama vile fonolojia ya kijaluo,kijerumani,kifaransa n.k.Fonetiki nayo huwa moja tu.

4.Fonolojia hushughulikia sifa za kiarudhi zilizo bainifu katika lugha husika na kutupilia mbali zile sifa zisizo bainifu katika lugha inayochunguzwa.

5.Wanafonolojia hukusanya tu sehemu ndogo ya sauti ya lugha fulani ilhali wanafonetiki h sauti nyingi kutoka lugha mbalimbali duniani.

6.Fonolojia huchambua sauti zilizo katika mfumo mmoja na lugha mahususi.Fonetiki huchunguza sauti za lugha kwa ujumla bila kuzingatia sauti hizo zinatumika wapi,vipi na kwa nini.

%d bloggers like this: