Ushairi

Nitabadilika.

NITABADILIKA
Natamani kuokoka, kabla sijaondoka.
Nikome kula mugoka, pesa nitoe sadaka.
‘Mechoka kucheza soka, ujana wangu mashaka.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

Nandika huno waraka, umfikie sidika.
Hiyo siku ya pasaka, tukuwe tumebadilika.
Ujana tupe talaka, tusiivuke mipaka.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

Nilirudie tabaka, kuona jami ya kaka.
‘Toe tope lojipaka, kwani ‘mekuwa kibaka.
Meharibika haraka, umri wa mamlaka.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

Kaya sijawajibika, Mama analalamika.
Machozi yanamtoka, kisa homu ‘metoweka.
Undugu umefutika, si waheshimu marika.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

Moshi pua yatifuka, bangi sigara nanuka.
Sheria nimekiuka, gereza natambulika.
Nywele kichwa ‘mesuka, Njiani wanamaka.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

Mimba yangu nimeruka, banati ‘lipomteka.
Mwanangu anazunguka, kusaka liyekiuka.
Mwisho mie nimefika, akilini natabika.
Nakubali ‘mepotoka, mie nitabadilika.

(Malenga:Lévis)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close