Nipende vile nilivyo.
NIPENDE VILE NILIVYO.
Bora kuliweka wazi, nisije nikaumbuka.
Usinitazame vazi, kasema mwema mkaka.
Haya mambo ya kizazi, hupita kila dakika.
NIPENDE VILE NILIVYO, USIPENDE VAZI LANGU.🤣🤣
Vichapo nina vichapa, kila tunapo kutana.
Kwa pasi ninazichapa, deti tunapokutana.
Mie mwenza sina pupa, nalisema na mchana.
NIPENDE VILE NILIVYO, USIPENDE VAZI LANGU 🤣🤣
Mwenza nina dhalilika, hadhi njema kujitwika.
Takataka nina saka, ni yangu kazi mi Kaka.
Na kwenu nimeshafika, kuja beba takataka.
NIPENDE VILE NILIVYO, USIPENDE VAZI LANGU.🤣🤣
Kutakata ninataka, licha ya kazi ni duni.
Nakutaka Muhibaka, usidhani ni utani.
Kwa wazazi tutafika, tumuombe RAHAMANI.
NIPENDE VILE NILIVYO, USIPENDE VAZI LANGU.🤣🤣
Nina liweka dhahiri, ili usije kujuta.
Kwa kweli litafakari, ukweli uneupata.
Akujaliye KAHARI, kwa mwengine Bebi futa.
NIPENDE VILE NILIVYO, USIPENDE VAZI LANGU.🤣🤣
(Mtunzi ni Said Mruu)