Ushairi

Nimenunua Bunduki.

Siri yangu nawapea,msiende kutangaza,
Mageni nawaletea,haya si ya vibaraza,
Wadudu nimekufia,siku hizi nashangaza,
Nimenunua bundiki,kulindia langu penzi.

Msiseme ni kihoro,ninapotongoa haya
Kitwani Sina kasoro,hazijaungua waya,
Yanichosha misururo,na zao tabia mbaya,
Nimenunua bundiki, kulindia langu penzi.

Vimada wanizaini,kumbe nia utalihi,
Nimamka nabaini,hiyo yote ni nishahi,
Ukiondoka hubani,fahamu nakukirihi,
Nimenunua bundiki, kulindia langu penzi

Mtima siyo uwanja,Kila Mara kuchezea,
Mdomo napaka wanja,pilipili wanitia,
Nimeujua ujanja,nawafunzeni tabia,
Nimenunua bundiki, kulindia langu penzi.

Kazini nina bidii,napanda napalilia,
Usemecho nitatii,hata mkongo kutia,
Kunitenda hulipii,bunduki yamalizia,
Nimenunua bundiki, kulindia langu penzi.

(Malenga ni Brian Bin Oigara)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close