Lugha na Sarufi

Ngeli za Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili ina ngeli nyingi sana.Baadhi yazo bado yafanyiwa utafiti na wataalam mbalimbali wa lugha ili kuidhinisha matumizi yake.K.m Ngeli ya VI-VI ambayo ina nomino nomino moja tu inayojumuishwa humo yaani vita.

Ngeli zinazotumika aghalabu ni kama zifuatazo.

 1. Ngeli ya A-WA-Hii ni ngeli ya vitu vilivyo na uhai kama vile wanyama,ndege, binadamu, wadudu n.k.Baadhi ya maneno yanaanza kwa kiambishi cha ngeli M(umoja) na Wa(wingi). Mengine huanza kwa Ki(umoja) na Vi(Wingi).Kuna miundo mingine mingi ambayo ipo katika ngeli hii.
 2. Ngeli ya LI-YA-Hii ni ngeli ya vitu visivyokuwa na uhai.k.m gari.Aidha ngeli hii hubeba majina yaliyo katika hali ya ukubwa.K.m janajike Majina mengi hapa huwa na muundo wa JI(umoja) na MA(Wingi).
 3. Ngeli ya KI-VI-Hii pia ni ngeli ya vitu visivyokuwa na uhai.Isitoshe,hubeba majina katika hali ya udogo.K.m Kijumba-Vijumba.Majina mengi hapa huanza kwa MA au ME katika wingi.
 4. Ngeli ya U-I-Nomino nyingi huanza kwa M(umoja) na MI(Wingi).Hii ngeli pia hubeba majina ya miti au mimea.K.m Mpera-Mipera
 5. Ngeli ya U-ZI-Majina mengi huanza kwa U(umoja) na ZI(wingi).Majina yenye silabi mbili huongezwa /ny/ katika wingi.Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa kiambishi cha ngeli U.
 6. Ngeli ya YA-YA-Ngeli ya nomino za wingi.Majina haya hayana umoja.Mengi yazo huanza kwa MA katika umoja na wingi.K.m Maji-maji
 7. Ngeli ya I-ZI-Ngeli hii hubeba majina yasiyobadilika katika umoja na wingi.Majina haya huchukua viambishi tofauti.Mengi yazo huanza kwa viambishi kama vile /ny/,/mb/,/ng/,/u/.
 8. Ngeli ya U-YA-Majina yaliyoko hapa huanza kwa U(umoja) na YA(wingi).
 9. Ngeli ya I-I-Hii ni ngeli ya majina ya wingi ambayo huchukua kiambishi I katika umoja na wingi vilevile.K.m Jua, mvua n.k.Majina haya hayana muundo maalum.
 10. Ngeli ya U-U-Hii ni ngeli ambayo majina yaliyomo huanza kwa U katika umoja na wingi.Kwa upande mwingine,kuna pia yale majina yasiyoanza kwa U katika wingi.K.m uzi-nyuzi, ugonjwa-magonjwa n.k
 11. Ngeli ya PA-KU-MU-Hii ni ngeli ya mahali/pahali.PA hudhihirisha mahali palipo wazi,KU hudhihirisha mahali kusikojulina ihali MU huonesha/humaanisha ndani kabisa.
Tags
Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close