Ushairi

Nani aliwaroga.

NANI AMEWAROGA?
Lipokuja divolusheni, kadhani sluhu mepata,
Usilojua Jamani, ni usiku wa matata,
Kura liwapigieni, gavana na maseneta,
Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga?

Meoza moja samaki, mtungo u mashakani,
Wananchi wamehamaki, magavana chunguzeni,
Mafisadi Kawasaki, pesa zetu okoeni,
Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga?

Sonko kumi milioni, taachama kwa Korane,
Mia mbili milioni, zi mfukoni mwa Korane,
Wakifika kortini, dhamana si Mara nne ,
Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga?

Ni makubwa ya Obado, ligawa na familiya,
Mehukumiwa Obado, ila pesa mesaliya,
Twalalamika si bado, pesa kuturudishiya,
Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga?

Kiti hiki Cha gavana, kisiwe hapo debeni,
Kwetu hakina Maana,bali kodi kwongezeni,
Tubakie kama Jana, ufisadi kupunguzeni,
Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga?

Beti sita ninatuwa, kalamu melalamika,
Lalamiko tumetowa, twatumai Mesikika,
Aliyewaroga hawa, wasamehe kwa hakika,
Wapate kuwajibika, ufisadi wakomeni.

(Chebet Lydia-Malenga)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close