Miundo Ya Silabi Za Kiswahili.

Kuna miundo mbalimbali za silabi za kama ifuatavyo.
1.Silabi za Irabu pekee k.v katika maneno kama vile oa na ua.
2.Silabi za K+I-Hapa ndipo maneno mengi ya Kiswahili yanapatikana.Maneno huwa na silabi moja, mbili au zaidi.Mifano ipo katika maneno kama vile mama,baba n.k
3.Silabi za K+K+I-Konsonanti za mwanzo katika muundo huu huwa na vitamkwa vya ving’ong’o/nazali.Mifano ya maneno ni kama ndevu,Mbacha n.k
4.Silabi za K+k+I-Hapa konsonanti huwa mwanzo kisha kufuatiwa na kiyeyusho na kumalizika kwa irabu.Mifano ya maneno yenye silabi za muundo huu ni kama vile mbwa,mwadhama n.k
5.Silabi za K+K+K+I-Muundo huu hushamiri katika maneno yaliyoswahilishwa/kukopwa kutoka lugha za Kigeni.Mifano ya maneno ni kama vile Skrubu n.k
6.Silabi za K+I+K-Maneno yaliyo na muundo huu ni yale ya kibantu au yaliyokopwa.Silabi funge hushamiri hapa sana.Mifano ya maneno ni kama vile labda, teknolojia n.k
(K inasimamia konsonanti,k inasimamia kiyeyusho (/w/ na /y/),I inasimamia irabu.