Ushairi

Mimba za mapema.

MIMBA ZA MAPEMA

HABARI ZENU WENZANGU, SALAMU NA WAPATIA.
NIWAJUZE WALIMWENGU, YALO KITHIRI DUNIA.
MADADA WANA MAJUNGU, NAOMBA MJE SIKIA.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA😭😢

LA KWANZA NALO CHANGIA, KWA HAWA WETU BANATI.
UKWELI WANAZEMBEA, UVIVU KUJIA KATI.
MENGI WAKIYASUSIA, WAKIINGOJA BAHATI.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA😭😢

LA PILI NI MAHITAJI, YAWASUMBUA AKILI.
AKIUKOSA MTAJI, ATAKWENDA KWA JAMALI.
AKIENDA ZAKE MAJI, ATAITISHWA AMALI.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

LA TATU NI KIFATIA, NI KUTENDEWA UNYAMA.
IDHINI HAJA ITOA, JANADUME LA SIMAMA.
LITAMZIBIA NJIA, NI USIKU WA MAPEMA.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

LA NNE NITALISEMA, ILA NA HOFU MOYONI.
CHANZO NI AKINA MAMA, HAWASEMI UFINGANI.
KWAO HUONA SHUTUMA, WATOTO KUAMBIANI.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

LA TANO UMASIKINI, PA KUBWA UNACHANGIA.
VISODO WAKITAMANI, KWA VIJANA HUENDEA.
WAPUNGUZE KUTAMANI, VYA GHALI VYA GARAMIA.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

LA SITA NASISITIZA, MAMBO YANAYO WASIBU.
WASIPENDE KUJIUZA, KATU ISIWE WAJIBU.
NAOMBA KUJITULIZA, WAPATE SOMA VITABU.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

KISIWA NAJIDONDOSHA, NAJITOWA JUKWAANI.
MAONGEZI YAMETOSHA, YAWAFAENI JAMANI.
WALA SI YAKUPOTOSHA, NAMUOGOPA MANANI.
MASAHIBU KUWASIBU, KUPATA MIMBA MAPEMA 😭😢

(MTUNZI:SAID MRUU)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close