Lugha na Sarufi

MCHANGO WA VYUO VIKUU KATIKA KISWAHILI.

MCHANGO WA VYUO VIKUU VYA KENYA KATIKA KUENDELEZA TAALUMA YA KISWAHILI.Kuna vyuo vikuu nyingi nchini Kenya vinavyofunza Kiswahili. Hivi ni pamoja na vyuo vya kiserikali na zile za kibinafsi. Kupitia kwazo Kiswahili kimepata Kuendelea na hata kuvuka mipaka na hata watu wengi kupata ajira. Wahadhiri wameweza kuajiriwa kila uchao, wanafunzi kupata nafasi ya kuandika nakala na maandishi mengi katika vyombo vya habari . Kwa hivyo, Kiswahili kama lugha imeweza kukua kama taaluma kwa njia nyingi.CHUO KIKUU CHA MOI.Chuo hiki ni mojawapo ya vyuo vikuu vya Kenya ambavyo ni vya serikali. Inchini Kenya, chuo hiki cha Moi hudhamini lugha ya Kiswahili kwa upana na marefu.
Chuo hiki cha Moi kilianzishwa mnamo mwaka wa elfu moja mia nane themanini na tano. Lengo kuu ilikuwa ni kufunza masomo ya kisayansi na teknolojia, lakini shughuli za kufanya Kiswahili mojawapo ya somo za kufunza chuoni Moi zilikuwepo. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Moi walitakiwa kutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano ya kila siku.
Kitengo cha Kiswahili katika chuo hiki kilianza mnamo mwaka wa 1987 ambamo lengo kuu ilikuwa ni kufunza ” Kiswahili and other African languages.” Baadaye wanafunzi wote waliofuzu vyema walikabithiwa vyeti, uzamili na uzamilifu katika lugha ya Kiswahili.
Kulingana na profesa Mbogo alisema kuwa Kiswahili kilifanywa rasmi mojawapo ya kozi ambayo ingefunzwa Moi mwaka 2002. Walimu wengi wa Kiswahili walifuzu vyema na hatimaye
Kulingana na gazeti la taifa leo, 2007 lililoandikwa na mwanahabari Titus Ominde, kongamano na la Kiswahili la siku tatu ilifanyika katika chuo kikuu cha Moi, bewa kuu la Kesses mjini Eldoret.
Kongamano hili lilihudhuriwa na wasomi pamoja na wataalam kutoka Afrika mashariki. Kongamano hili lilikuwa limefadhiwa na chama na chama cha Kiswahili cha taifa ( CHAKITA) na idara ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika katika chuo kikuu cha Moi.
Lengo kuu la kongamano hili ilikuwa kujadili umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika mshikamano wa kitaifa na uwiano barani Afrika Mashariki.Mmoja wa waandilizi wa kongamano hilo ni kama Daktari Allan Opijah alifichua kuwa mbali na kujadili mbinu bora za kuboresha lugha ya Kiswahili. Kongamano hilo linalenga kutoa changamoto kwa serikali kukumbatia lugha hiyo katika juhudi za kuimarisha uwiano miongoni mwa wakenya wa matabaka mbalimbali.
Katika chuo kikuu cha Moi kuna chama cha Kiswahili cha Moi (CHAKIMO).Chama hiki kina wanafunzi wasomi ambao hupata fursa ya kujadiliana na kushauriana kuhusu kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Kenya.Chama hiki hutetea na kuleta maendeleo katika taaluma ya Kiswahili na huduma zake za Kimaendeleo nchini Kenya.Aidha,wanafunzi hupata fursa ya kuchangia masuala ya sera na mipango ya lugha ya Kiswahili huku mara nyingi wakipata mafanikio ya kufana.Pia chama hiki huangazia masuala yanayohusiana na utunzi wa kisanaa kama vile nyimbo na mashairi.Tungo hizi za kisanaa zimeweza kuchapisha katika jarida la DAFINA LEO ambalo hutolewa kila wiki.Waandalizi wa kongamano hilo wakihutubu kutoka mjini Eldoret, chuo kikuu cha Moi, walitaka serikali kuwa na bajeti maalum ya kuboresha lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Kwa ujumla chuo kikuu cha Moi, imechangia kukuza taaluma ya Kiswahili nchini Kenya na hata mataifa mengine. Walimu wengi wa Kiswahili wamefuzu kutoka chuo kikuu cha Moi pamoja na waandishi gwiji wa nakala za Kiswahili.CHUO KIKUU CHA NAIROBI.
Kiswahili hufunzwa kama somo katika chuo kikuu cha Nairobi. Hufunzwa kama kitengo ” linguistics and African languages” kilichoanzishwa mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa na sabini (1970). Kitengo hiki huchunguza Kiswahili kwa kina . Wanafunzi waliokuwa katika kitengo cha Kiswahili walifunzwa Kiswahili kwa kutumia lugha ya kimombo hata hivyo baadaye linguistiki ilifunzwa kwa lugha ya Kiswahili.Kiswahili kinaendelea kukua sana katika chuo kikuu cha Nairobi haswa kikuyu ambapo kimeibua walimu wengi wa lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wanaosomea cheti cha ualimu kitengo cha Kiswahili na wanaofanya uzamili katika Kiswahili ufunzwa na waadhiri katika lugha ya Kiswahili. Kupitia sababu hii chuo kikuu cha Nairobi kimechangia vikali kukua kwa lugha ya Kiswahili, kwa hivyo tunawapongeza walimu wa Kiswahili katika chuo kikuu cha Nairobi.Kuanzia kwa idara ya Kiswahili katika chuo hiki cha Nairobi pia kulichangia kuanzishwa kwa chama cha Kiswahili cha Nairobi ( CHAKINA). Chama hiki kimeweza kukuza Kiswahili kupitia kwa jarida lake ambalo huchapishwa mara kwa mara na kuangazia vipengele tofauti vya lugha kama vile ushairi na sarufi. Aidha hiki kimeweza kupanga makongamano na warsha mbalimbali za kukuza lugha ambapo wataalam hualikwa ili kuja kuzungumza na wanafunzi pia hushiriki katika mijadala inayofanyika kila wiki hivyo kupanua uwezo wao wa lugha.Idara ya Kiswahili imekuza waandishi wengi kutokana na uchapishaji wa makala,vitabu na hata tasnifu mbalimbali. Maandishi haya yameangazia vipengele mbalimbali vya lugha. Tunapozungumzia waandishi tunamaanisha hata wanafunzi na waadhiri. Waadhiri waliokuza vipaji vyao vya uandishi ni pamoja na profesa Mohammed Abdulaziz, profesa K.w. wamitila, profesa Kithaka wa Mberia, profesa John Habwe, Daktari Mukhwana, Daktari Iribe Mwangi pamoja na wengine wengi. Makala yao yaliyochapishwa yametumika katika shule za msingi, sekondari na hata vyuo vikuu vingine kufunza lugha. Kwa mfano, Kuna vitabu vingi vya hadithi fupi, riwaya na tamthilia zilizoandikwa katika shule za sekondari zilizoandikwa nao. Kwa mfano ‘Darubini ya Kiswahili kilichoandikwa na John Habwe, Assumpta. K. Matei kinatumiwa kama kitabu cha kiada., kupitia kwa ushirikiano na vyuo vingine, chuo hiki kimeweza kuhudhuria makongamano ya kukuza Kiswahili . Kwa mfano, kongamano la kitaifa la CHAKITA lililoandaliwa Katika chuo kikuu cha Karatina mwaka 2019 kauli mbiu ikiwa ni ‘ Kiswahili na maendeleo Endelevu’ ambapo wameweza kuchangia mada hii na kupata kuzungumza na wataalam mbalimbali. Aidha, imeshirikiana na chuo kikuu cha Bayreuth cha ujerumani ambapo wanafunzi kadhaa wameweza kupata nafasi ya kusomea shahada ya uzamili na hata uzamifu.
Chuo hiki pia kimesaidia wanafunzi katika nyanja mbalimbali baada ya kukamilisha madomo. Wengine wamepata nafasi ya kutafsiri, wengine wameweza kuwanwatangazaji na wengine wamekuwa waadhiri.Ni wazi kwamba chuo hiki kinachotambulika ulimwenguni kwa ubora wa mafunzo kimechangia. Pakubwa katika kuendeleza taaluma ya Kiswahili kupitia kwa hatua anuwai ambazo idara yake imepiga.
Aidha, wahadhiri wa chuo hiki wamepata nafasi ya kuendeleza na kukuza Kiswahili kwa redio na katika runinga. Baadhi yao wamealikwa mara si moja kuangazia vipengele mbalimbali vya lugha kama vile katika kipindi cha Nuru ya lugha katika stesheni ya Redio ya Radio maisha.
Aidha, wanafunzi ambao hutia fora katika uandishi wa makala ya Kiswahili hupata nafasi ya kutunzwa na kuhimizwa kukuza vipaji vyao.CHUO KIKUU CHA KENYATTA.
Taaluma ya Kiswahili ilianzishwa chuoni Kenyatta mwaka wa 1987 chini ya idara ya Kiswahili na lugha za Kiafrika. Kuanzishwa kwake kulichangia kuanzishwa kwa chama cha Kiswahili cha Kenyatta ( CHAKIKE).
Kupia kwa CHAKIKE, wanafunzi na hata waadhiri wameweza kushiriki katika kongamano mbalimbali za kukuza Kiswahili kama vile kongamano la CHAKAMA ( chama cha Kiswahili cha Afrika mashariki) iliyofanyika nchini Tanzania mwaka uliopita. Waadhiri wa Kiswahili, Daktari Pamela Ngugi na Daktari Miriam Osore pamoja na wanafunzi wa pHD wa kutoka Uganda : Abdu Salimu Rais na Yunus Lubuuka katika kongamano la CHAKIDU katika chuo kikuu cha Kyambogo.
Idara ya Kiswahili chuoni humo baadaye ilianzisha maktaba ndogo ambamo sasa mnahifadhiwa vitabu, majarida na tasnifu za Kiswahili. Kupitia kwa hili, wanafunzi wamewezeshwa kufanya tafiti zao kwa njia iloyo shwari. Wanafunzi pia hutumia maabara ya lugha ya chuo Katika tafiti hasa za kiisimu.Wahidhini chuoni humu wameshirikiana na waadhiri wengine kutoa vyuo vingine kama vile Moi na Nairobi katika kufanya utafiti mbalimbali kuhusu vipengele maalum vya Kiswahili. Kupitia kwa ushirikiano huu, vitabu kadhaa vimeweza kuchapishwa ili kusaidia wanafunzi katika masomo. Kwa mfano ‘ Chacha ( 2019) ” Tathmini ya mitandao ya WhatsApp katika ukuzaji wa Kiswahili katika John Kobia na wengine ( wah). Uwezeshaji wa Kiswahili kama wenzo wa maarifa.”
Isitoshe, baada ya kumaliza masomo yao, wanafunzi huajiriwa katika nyanja mbalimbali na kuwa walimu,wahariri, wanahabari, wafasiri, wakalimani namengine mengi. Wanafunzi pia huandika makala kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili vinavyochapishwa katika magazeti mbalimbali ya Kiswahili kama vile K.U T.VAidha, mfano wa mafunzo chuoni umechangia uandishi wa tafrifu nyingi zinazosaidia kupanua mawanda ya lugha.
Kiswahili kilifanywa kama somo la lazima baada ya Tume ya Mackay ilichangia kuanzishwa kwa chuo hiki kilihimiza katika ripoti yake hivo. Hii ni kwa kuwa wanafunzi wengi waliofuzu kutoka chuoni hawakuweza kujieleza kwa ufasaha katika lugha ya Kiswahili.
Kiswahili kama taaluma pia imeendelezwa kupitia ushirikiano na vyuo vya nchi za kigeni kama vile chuo cha Michiguu state cha marekani ambapo waadhiri wa vyuo vyote viwili wametayarisha warsha ya kukuza lugha ya Kiswahili.
Wanafunzi wamepata fursa ya kualikwa kwenye vipindi mbalimbali redioni na katika runinga kwa minajili ya kukuza lugha. Hapa wao hupata nafasi ya kughani mashairi na kushiriki katika vitengo mbalimbali kama vile chemshabongo. Kwa mfano katika runinga ya KTN News.
Wanafunzi hupewa nafasi ya kuendesha vipindi mbalimbali kwa kutumia lugha ya kiswahili katika chuo hiki (Runinga ya K. U .T V)Mafunzo ya walimu wa Kiswahili katika shule za msingi yalianza kuendeshwa wakati wa likizo ambapo kozi maalum za Kiswahili zilianzishwa. Hapo chuo Kikuu kishirikishi cha Kenyatta kilianzisha kozi ya kuwapandisha walimu vyeo kuanzia mwaka wa 1978.Kupitia kwa kitengo cha fasihi, wanafunzi hupewa fursa ya kuigiza, kuimba nyimbo, kucheza ngoma, kufanya utani na mambo mengine mengi yanayohusu utamaduni wa jamii za Kiafrika. Haya yote hufanywa kutumia lugha ya Kiswahili.

Tags
Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close