Lugha na Sarufi
Matumizi Ya Kiambishi Na.
Kiambishi ‘na’ hutumika kwa njia tofauti katika sentensi ili kuonyesha maana mbalimbali kama ifuatavyo:
- Hutumika kuonyesha dhana ya wakati uliopo.K.m Mama anapika chakula.
- Hutumika kama kiunganishi katika sentensi.K.m Neema na Fadhili wanacheza mpira.
- Hutumika kuonyesha dhana ya umilikaji.K.m Juma ana kalamu nzuri.
- Hutumika kuonyesha mtendaji wa kitendo.K.m Mpira huo ulipigwa na Mwadime.
- Hutumika kuonyesha kauli ya kutendana na kutendeana.K.m Jana wanamasumbwi walipigana kwenye uwanja wa Tononoka/Wanafunzi walipigiana kelele.
- Hutumika kuonyesha hali.K.m Yule mjane ana huzuni baada ya kifo cha mumewe.
- Hutumika kufupisha nafsi.K.m Nao waliendelea kucheza densi.