Ushairi
Mashairi Ya Tarbia.
TAKUENZI MOYONI.
Moyoni uwe peke yako, wewe kipenzi cha moyo.
Nakupenda pekeako, hakuna mwingine huyo.Ila nasema ni kwako, wengine ni sagamoyo.
Pendo letu limoyoni,takuenzi aushini.
Kwako mimi sibanduki,chaguo langu la moyo.
Kwingine mimi sitaki,ni wewe kipenzi changu.
Kama asali ya nyuki, napenda uwe wa kwangu.
Pendo letu limoyoni, takuenzi aushini.
Hatimaye lije zaa, matunda mazuri pendo.
Mahari tapelekea, yenye mazuri muundo.
Wa kwako watapokea, mahari kwa mdundo.
Pendo letu limoyoni, takuenzi aushini.
Akidi tafanya sisi,kanisani pale mbele.
Atakuwepo kasisi tukinyweshana kwa dele.
Pete visha ‘we mapisi,tutapendana milele.
(Mwalimu Bosire.D.Onsongo,bosiredaniel12@gmail.com)