Ushairi

Mapacha.

MAPACHA
Saidi….
Samahani dada yangu, naomba ukweli wako.
Usidhani ni majungu, karusha mikono yako.
Sema ukweli dadangu, nije ni juwe mwenzako.
MAPACHA MWANITATIZA, SI MAJINA BALI SURA.

Mebibi…
Kakangu ninakwambia, ulo ukweli sikia.
Na wala sitochukia, kakangu kukupuzia.
Ukweli unatakia, ni upi bu nijuzia.
MAPACHA TUJAFANANA, ILA UJATUZOEA.

Saidi…
Dadangu mumeniweza, kweli nitawajuzia.
Licha ya najiuliza, kisura mwanizengua.
Naiona miujiza, sijui wapi anzia.
MAPACHA MWANITATIZA, SI MAJINA BALI SURA.

Mebibi…
Acha kujilizaliza, eti sie hutujui.
Na sana twakutatiza, ebu acha kuenjoi.
Wala sio miujiza, kweli wewe haujui.
MAPACHA TUJAFANANA, ILA UJATUZOEA.

Saidi…
Wajuwa nikita Mamu, Mebibi anaitika.
Hata kama ni salamu, nyote mnapaitika.
Ukweli siwafahamu, mwanizuzua mkaka.
MAPACHA MWANITATIZA, SI NAJINA BAMI SURA.

Mebibi…
Wanichekesha kakangu, kwa unavyotatizika.
Sura ya Mamu na yangu, zisikutatize hakika.
Tazama vyema ndu yangu, wala si fanye haraka.
MAPACHA TUJAFANANA, ILA UJATUZOEA.

Saidi…
Wewe unanidanganya, Mapacha wanafanana.
Wanalijua wakenya, maneno wayatafuna.
Tena mie nakukanya, usambe nakutukana.
MAPACHA MWANITATIZA, SI MAJINA BALI SURA.

Mebibi…
Ngoja taka nikutoa, mapacha hawafanani.
Kunayo siri sikia, ambayo hutokezani.
Wakenya hawajajua,hii ni siri sirini.
MAPACHA TUJAFANANA, ILA UJATUZOEA.

Saidi…
Ubishani siutaki, nitumie picha zenu.
Initoke na hamaki, kibaini macho yenu.
Pia kama hamtaki, nitatulia mwenzenu.
MAPACHA MWANITATIZA, SI MAJINA BALI SURA.

Mebibi…
Wala sina ubishani, kuhusu hilo jamani.
Na picha naitumani, ukweli ufahamuni.
None Kama tajuani, siri yetu we mwendani.
MAPACHA TUJAFANANA, ILA UJATUZOEA.

PAMOJA………..
Sawa tutazame picha, kwa pamoja ndugu zangu.
Tuleni nao mchicha, wafahamu walimwengu.
Wala hakuna kuficha, tumejuana nwenzangu.
NATUMAI TWAJUANA, TOFAUTI TWAIONA.

(WATUNZI:SAID MRUU NA MEBIBI BAKARI)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close