Ushairi

Majina yanasadifu.

Kila jina lina mana, vipi yakwako wajua /
Haitakuwa na mana, kuitwa usichojua /
Wazi ama fichikana, maana kuitambua /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Tuitaneni mazuri, pia tunayoyapenda /
Maana zilizo nzuri, siyo yale yanoranda /
Mola alitushauri, majonzi kwa walosanda /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Yapo yanayosadifu, ubora na mapungufu /
Sitake piga turufu, mwite mja wa Raufu /
Wakwako ukubalifu, taruhani utiifu /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Utobwe ukaukifu, Rabbana atakuafu /
Takwepana na uchafu, ungangari kama #Sefu /
Majanga kwo uchechefu, kua lulu ka sarafu /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Majina yalo mazuri, husadifu kuwa mwema /
Kukupa bishara nzuri, epukana na dhahama /
Ukafikwa na mazuri, umshukuru karima /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Majina yalo mabaya, waitwao ni majanga /
Katu hawanaga haya, ugegedu wautinga /
Wakaapo wanapwaya, jina baya wewe pinga /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////
*
Waitwa jina siafu, wawaza tu masurufu /
Hufanyi kama awafu, hunalo linosadifu /
Jina mana yakinifu, ubora na upungufu /
Majina yanasadifu, chunguza utabaini ////

(Malenga ni Bin Omary)

Show More

Related Articles

3 Comments

 1. Excellent blog you have here but I was curious about if
  you knew of any message boarrds that cover the same topocs
  discussd in tbis article? I’d really like to bbe a part of group where I can get ffeedback from other knowledgeable people that share the same interest.
  If you have any recommendations, please let mme know.
  Bless you!
  https://howtowriteapersonalessayforscholarships.wordpress.com/multiple-essay-writing-services-online
  best exsay writing services
  best essaay writing services https://scarlet-lette7352.hpage.com/buy-a-term-paper-of-top-quality.html

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close