Ushairi

Maadamu umeniacha

MADAMU UMENIACHA.

Mi sijawahi kupenda, kama nilivyo kupenda.
Leo umesha nitenda, tena ukanamba kwenda.
Kumbe mitili ya Punda, ulitaka mi kukonda.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

Unakumbuka mwenyewe, ulipo ni tamkia.
“Nimekupenda mwenyewe, toa hofu maidia.
Hivi wanipa kiwewe, vibaya kunisemea.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

Ni kikumbuka ya nyuma, mabusu kuniptia.
Nina shindwa kusimama, mwili una nyong’onyea.
Kwa kweli inaniuma, kidonda naugulia.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

Imfikiye habari, ye fulani mwana Ali.
Machozi yanitiriri, mwenziwe mi sina hali.
Akapiga msitari, mapenzi kwake muhali.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

Mwenziwe ameniweza, moyoni nimepaniki.
Nimebaki nikiwaza, kumbe alitaka kiki.
Hi ngoma hatoiweza, lazima atiye tiki.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

Sasa najiamulia, kupenda kwake ni basi.
Na nyuma sitorudia, na kwenda kama risasi.
Nako mbali kifikia, natuwa yangu nafusi.
PENZILO SILO LA KWELI, MADAMU UMENIACHA.💋🥀

(MTUNZI: SAID MRUU)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close