Ushairi

Gimba.

GIMBA
Gimba lisilo akili, huwa linaitwa gogo,
Mambo yake mushkeli, huishia kwa kipigo,
Halifanyi tasihili, mpaka lizuwe zogo,
Dude hili si jalili, mamboye yenda upogo.

Linaitwa limbukeni, lipendalo ushaufu,
Linatekwa halioni,haliishi majisifu,
Kiliona Li mbioni, kana kwamba Li
turufu,
Dude hili si jalili, mamboye yenda upogo.

Silambiye yako siri,litasema hadharani,
Tena fanya tahadhari, litakutosa demani,
Katu halina nadhari, liko kama punguwani,
Dude hili si jalili, mamboye yenda upogo.

Lina maneno matamu, yalosheheni uongo,
Kilipatiya salamu, latongowa kwa maringo,
Kilipenda ufahamu, hili takupa ukongo,
Dude hili si jalili, mamboye yenda upogo.

Nakusihi tamakani, usije paliwa moto,
Siliweke mtimani, litakupa changamoto,
Litakupa mitihani, uliye kama mtoto,
Dude hili si jalili, mamboye yenda upogo.

(MTUNZI: JOSHUA PHILLIP)

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button
Close
Close