Lugha na Sarufi
Dhana Ya Fonetiki.
Hichi ni kiwango cha lugha kinachoshughulikia sauti za lugha ya mwanadamu kwa ujumla.
Taaluma hii kuchunguza namna sauti anuwai ama za irabu au konsonanti hutamkwa kinywani mwa mwanadamu.
Katika fonetiki, mwanaisimu huchunguza viungo vinayoshiriki katika utamkaji wa sauti yaani foni.Hujibu maswali yafuatayo:
1.Sauti za lugha ya mwanadamu ni ngapi na ni zipi?Sauti hizo ni nyingi na kuna nyingine ambazo hazijatafitiwa.
2.Sauti za lugha ya mwanadamu hutamkwaje na wapi? Kila mojawapo ya sauti hizo hutamkiwa mahali pake na kwa namna ya kipekee.
3.Foni za lugha ya mwanadamu zinasheheni sifa gani.Mwanaisimu anapochunguza taaluma hii huchambua sauti mbalimbali pasi na kujali zinatumiwa wapi,nani na kwa dhima zipi.