Fasihi

FASIHI.

Fasihi ni sanaa iwe ya uandishi au mdomo inayowasilisha ujumbe unaolenga maisha ya binadamu Kiufundi kwa kutumia mbinu anuwai za lugha.Hueleza hisia za mtu kwa kutumia vielelezo vyenye dhana maalum.

1.Fasihi ni sanaa kwa kuwa matukio hupangwa kiufundi ili yaweze kuwasilishwa vema kwa jamii husika.

2.Usanaa wa fasihi pia hujidhihirisha katika jinsi mambo yanavyoelezwa.Kuna ufundi fulani unaotumiwa kufikisha ujumbe kwa hadhira.K.m Ujumbe huweza kufichwa katika shairi, mafumbo,vitendawili n.k

3.Ujenzi wa wahusika pia huonyesha usanaa wa fasihi madhali wahusika huwa na tabia zinazotofautiana kati yao na mtunzi ndiye huamua mhusika fulani atawasilisha tabia ipi.

https://www.kiswahilishirafu.guru

4.Ni dhahiri pia mandhari ambamo fasihi hujengwa inaonesha usanaa wa fasihi kwa kuwa hujengwa Kiufundi ili yasaidie kuikamilisha kazi ya fasihi.

5.Lugha pia huteuliwa kiufundi.Lugha hii hupambwa kwa kutumia nahau, misemo,methali, taswira, ishara na tamathali nyingine za semi.Hii hulenga kuibua hisia mseto kwa hadhira.Hii pia pia inaonyesha usanaa wa fasihi.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close