Hizi ni mbinu za Kiufundi zitumikazo na mwandishi/msimulizi wa kazi yoyote ya fasihi ambayo humlazimisha msomaji/hadhira kuisoma hadithi nzima ili kuzitambua.
Baadhi yazo ni kama vile:
Sadfa-Hii ni hali ambapo matukio hutendeka kwa pamoja bila ya kupangwa.Kisengerenyuma-Hapa mwandishi hurejelea matukio yaliyofanyika nyuma.Hivyo humlazimu kubadilika wakati kuyasimulia tena.Kisengerembele-Hapa mwandishi husimulia mambo yatakayotokea siku za halafu kwa kubadilisha wakati wa masimulizi.Njozi-Hapa mwandishi hutumia ndoto kujaribu kufichua yaliyotendeka/yatakayotokea katika masimulizi/hadithi yake.Upeo wa juu-Hapa mambo hufanyika kulingana na matakwa ya hadhira.Upeo wa chini-Hapa mambo hufanyika kinyume na matarajio ya hadhira.Mara nyingi hutokea baada ya upeo wa juu.Kinaya-Hii ni hali ambapo mambo hufanyika kinyume na matarajio katika hadithi.Kejeli-Hapa kuna matumizi ya maneno ya dharau kwa madhumuni ya kukashifu kitendo fulani/mtu fulani katika hadithi.Taharuki-Hii ni hali matukio ya hadhira/masimulizi humwacha msomaji/hadhira kinywa wazi na kumpatia hamu ya kutaka kusoma zaidi.Aghalabu hujitokeza paruwanja mwishoni mwa hadithi.