Fasihi

Fani Za Lugha Katika Fasihi.

Fani ni jinsi mambo yanavyosemwa katika fasihi.Yaani ni kipengele katika uwanja wa fasihi kinachojihusisha na umbo la nje la fasihi.Fani za lugha katika fasihi ni kama zifuatazo:

1.Takriri-Hii ni mbinu ya kurudiarudia sauti,silabi,neno au maneno kwa nia ya kusisitiza jambo fulani.K.m Awali ni awali hakuna awali mbovu.Neno ‘awali’ limerudiwa.

2.Taswira-Hii ni picha ya fikra zinazojengeka akilini mwa mtu baada ya kusoma, kusikia ama kushuhudia jambo fulani.

3.Udamisi/Chuku-Hii ni mbinu ya kukipa kitu sifa zaidi ya kiwango kinachokipasa kupewa.

4.Tashihisi-pia hujulikana kama uhaishaji.Hapa kitu hupewa sifa/uwezo za kitu kilicho hai k.v binadamu.k.m Nilitamani ardhi inimeze siku hiyo!

4.Balagha-Haya maswali yasiyohitaji jawabu na huwa na lengo la kumfikirisha mtu.

5.Kinaya-hii ni hali ambapo mambo yanatendeka kinyume na matarajio.

6.Ishara/Taashira-hii ni hali ya kitu fulani kuashiria kingine.

7.Tanakuzi-mbinu hii hutumika pale ambapo kauli/maneno yanapingana.

8.Kejeli/stihizai-hii ni mbinu ya kufanyia mtu utani/mzaha kwa madhumuni ya kupinga tabia zisizofaa.

9.Tashbihi/Tashbiha-Hii ni usemi wa mlinganisho au ufananisho wa vitu viwili kwa kutumia maneno kama vile kama, mithili ya, mfano wa,tamthili ya n.k.K.m Yeye ni mrefu kama mlingoti.

10.Sitiari-Hii ni kinyume cha tashbihi.Hapa vitu hulinganishwa bila kutumia maneno ya kulinganisha.K.m Baba ni simba.Hii ina maana baba ni mkali kama simba.

11.Tanakali za sauti-Hapa sauti za vitendo au vitu huigwa.K.m Alianguka chini pu!

12.Methali-Hizi ni semi za kimapokeo ambao hutoa kauli za kuonya, kuelimisha au kupongeza kwa njia ya busara.K.m Hasira hasara.

(Fani ya Fasihi simulizi kwa shule za upili,Assumpta .K. Mateo,Kamusi kuu ya Kiswahili, Longhorn publishers)

Tags
Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Back to top button
Close
Close