Skip to content

Category: Ushairi

Shairi la ukaraguni.

Tumekosa Nini? Mungu muumba dunia, mimea na wanadamu, Nimekuja nikilia, pasi kujali kaumu, Wewe ndiwe waridhia, pita nasi hali ngumu, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Kamwe uwezo hatuna, tungeishika dunia, Tuweze kutakasana, mawele sijeingia, Na hongo tungepeana, hasa kwa korona pia, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Yarabi tumejifunga, kwa vyumba pasi kutoka, Hata na hewa kupunga, mekuwa shida hakika, Halafu kutangatanga, pia imezuilika, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Au wafundisha nini, tuweze kulifahamu, Magoti tupige chini, kwa toba situhukumu, Tughofire kwa yakini, kwa korona loharamu, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini.… Read more Shairi la ukaraguni.

Mashairi Ya Tarbia.

TAKUENZI MOYONI. Moyoni uwe peke yako, wewe kipenzi cha moyo. Nakupenda pekeako, hakuna mwingine huyo.Ila nasema ni kwako, wengine ni sagamoyo.Pendo letu limoyoni,takuenzi aushini. Kwako mimi sibanduki,chaguo langu la moyo.Kwingine mimi sitaki,ni wewe kipenzi changu.Kama asali ya nyuki, napenda uwe wa kwangu.Pendo letu limoyoni, takuenzi aushini. Hatimaye lije zaa, matunda mazuri pendo.Mahari tapelekea, yenye mazuri muundo.Wa kwako watapokea, mahari kwa mdundo.Pendo letu limoyoni, takuenzi aushini. Akidi tafanya sisi,kanisani pale mbele.Atakuwepo kasisi tukinyweshana kwa dele.Pete visha ‘we mapisi,tutapendana milele. (Mwalimu Bosire.D.Onsongo,bosiredaniel12@gmail.com)

Istilahi za ushairi.

Kuna misamiati mingi ambayo hutumika katika ushairi. Mazda-Hii ni kuongeza silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani. Inkisari-Hii ni kupunguza idadi ya silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani. Dhamira-Hii ni lengo au nia ya mtunzi wa shairi. Maudhui-Hii ni ujumbe unaojitokeza katika shairi. Utohozi-Hii ni kuswahilisha maneno.K.m Facebook-fesibuku. Tabdila-Hii ni kubadilisha silabi ya mwisho ya neno bila kuathiri idadi ya mizani. Ukiukaji wa sarufi/kuboronga lugha.K.m Anapika mama chakula badala ya mama anapika chakula.

Shairi la Arudhi.

Safiri Salama Rais Mstaafu Moi. Huzuni ‘nayo Moyoni, sisi Kama wanakenya Alfajiri huzuni,baba Moi kafariki Tutakutia wazoni, Ni mengi uliyatenda Rais mstaafu Moi,safiri salama uko Hatuna pia matata,kila kitu ni bayana Hulikataa ka’kata,kutenganisha wakenya Wanakenya tulidata,Moi kaboresha kenya Rais mstaafu Moi, Safiri Salama uko Mashule uliyajenga, mazahanati tunayo Wakenya hata makanga ,maziwa nyayo wakanywa Barabara alijenga,maendeleo kafanya Raise mstaafu Moi, Safiri Salama Uko (bosiredaniel12@gmail.com)