Skip to content

Category: Ushairi

Mashairi Kuntu ya Kiswahili.

.DONGO Dango – shabaha, lengo Dingo – Aina ya mdudu Wakongo – wagonjwa Tengo – chengo, aina ya samaki Mongo – mgongo Banango – uharibikaji Ngongongo – Tanakali ya sauti ya kitu kinachogongwa Narusha dongo kwa dango, dingo lisende majongo Lengo naliwe mpango, nisambe usongombwingo Namwamba mwendo kibyongo, mwenye khuluka ya ungo Dukale lifingwe fingo, asali sipigwe zongo Ayasitiri maungo, pamwe ulivyo ubongo Sehemu zilizo pango, ziwe ndani ya kifungo Atahadhari na mwengo, mingi inayo matongo Dukale lifingwe fingo, asali sipigwe zongo Duniya ni mviringo, ya panda shuka viwango Imesheheni… Read more Mashairi Kuntu ya Kiswahili.

Mashairi aula ya Kiswahili.

SHAIRI: USINIHUKUMU 1. Unionapo njiani, mikono narusharusha Usicheke asilani, na ubaya kunivisha Hulijui la moyoni, linalonihangaisha Kamwe usinihukumu, nawe hutohukumiwa 2. Usiniseme vibaya, kinyume ninapotenda Usinione mbaya, ni dunia yaniponda Yanisukuma pabaya, na maisha kunishinda Kamwe usinihikumu nawe hutohukumiwa 3. Vibaya nikiamua, usije kunihukumu Nikichukua hatua, hatua iso muhimu Usinihikumu pia, moyoni utie sumu Kamwe usinihikumu nawe hutohukumiwa 4 Nina yanonisumbua, moyoni yanonitesa Mawazo kunipatia, na furaha kuikosa Mengi kuyakosea, kwa hali inonitesa Kamwe usinihukumu, nawe hutohukumiwa 5. Usije ukanikashifu, unionapo njiani Useme ni mharifu, kunitia hatiani Hakuna mkamilifu, Papa… Read more Mashairi aula ya Kiswahili.

Mashairi bora ya Kiswahili.

UKIANGUKA MKUYU Mama kumbi za sherehe,pindi tunapofurahi Mama tupa starehe,atufanya twafurahi Mama niwakusamehe,huwa mtu sahihi Mkuyu ukianguka,wana wa ndege huyumba Mama ndiye huwa duwa,pindi tuwapo mbali Mama huwa muelewa,msimamo hubadili Mama tukipitiliwa,mazito huyakabili Mkuyu ukianguka,wana wa ndege huyumba Mama ndiye letu jiko,pindi napohisi njaa Mama ndo mshika mwiko,vyakula kuviandaa Mama ndiye hangaiko,kutulisha atufaa Mkuyu ukianguka,wana wa ndege huyumba Mama ni hospitali,wagonjwa tunapokuwa Mama ndo mwenye kujali,kwa kutupatia dawa Mama huwa hawi mbali,tunapomhitaji huwa Mkuyu ukianguka,wana wa ndege huyumba Maadamu tuna mama,kwake sisi ni watoto Tumpe zake heshima,sije katuchapa fito Asije… Read more Mashairi bora ya Kiswahili.

Mashairi bora ya Kiswahili.

Nisifu nikiwa hai, Nisikie nifurahiUsingoje nizirai, ama kifo kiniwaiSifa zako anuwai, Nikifa hazinifahiNizike ningali hai. Unisifu nikinai, kwa furaha nijidaiKuongeza ni jinai, Sema kweli si madaiSitazua vurumai, bora uwe huadaiNizike ningali hai. Msaada sikatai, Sizioni zenu chaiKwa taabu sijifai, mko kimya ngali haiKaburini kirishai, michangoni mwajidaiNizike ningali hai. Suti Kali yenye tai, Mwanivisha na si haiMara pilau kwa yai, Munakula walaghaiSifa zenu sizivai, Sijimanyi mi ‘Mgai’Nizike ningali hai. Wala hamujishangai, Mlikuwa hamufaiLeo sinao uhai, Kunijali mwajidaiSifa zenu hazijai, Kaburini hazikaiNizike ningali ngai. Tafadhali nawarai, Nifaeni ngali haiKama Ng’ombe na Masai,… Read more Mashairi bora ya Kiswahili.

Shairi la Maringo ni ya nini.

MARINGO NI YA NINI? Una damu mishipani, nyekundu kama ya kwangu,Kuishi u duniani, huishi kwenye mawingu,Uyaalayo nadhani, ndo tofauti na yangu,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Unywapo chai maziwa, kwangu nile mkandaa,Sharubati unapewa, nionapo nabung’aa,Japo hapa napagawa, kila siku ni dagaa,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Mavazi unovalia, yametolewa Japani,Yanakushika sawia, siyo kama yangu duni,Matumbani kiingia, bei yangu ishirini,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Yangu duni hudumu, ila yote huzeeka,Yachanikapo haramu, yatupwa kwenye vichaka,Mwenzio hana hamu, zote za deki hakika,Hayo maringo ya nini, ulonayo hayadumu. Ulivyonunua gari, hatupumui wenziyo,Mambo kwetu… Read more Shairi la Maringo ni ya nini.

Shairi la Kizuri chavutia

KIZURI Kizuri kinavutia, moyoni hata ozini,Yeyote hujitakia, kwa vyovyote maishani,Waja wajitafutia,kazini au nyumbani,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Kizuri chang’ang’aniwa, masikini na tajiri,Popote chapiganiwa, jambo hili siyo siri,Wengi wachanganyikiwa, njiani wakisafiri,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Uwe hata ni mwalimu, uhodari ni gharamu,Ukakamavu dawamu, kujituma ni lazima,Lazima ujilazimu, kuiboresha huduma,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Awe ni mke wandani, wapo wa kategoria,Yule hodari jikoni, kisura na kitabia,Popote hapatikani, ni adimu nawambia,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Kizuri chataka muda, bidii pasi kukoma,Namba wani jitihada, kwenye bonde na milima,Kwenye raha hata shida, mazuri yataka wema,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. (Toney… Read more Shairi la Kizuri chavutia