Skip to content

Category: Ushairi

Umalenga ni basi.

UMALENGA NI BASI Moyo wangu umegoma, kutunga tena sidhani Ushairi nauhama, malenga sina thamani Bongo nalo limekwama, tungo hawazitamani Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Yani kote makundini, tungo zangu hazisomwi Hata kule ulingoni, japo ya mbwa siamwi Kule kwetu kisimani, naliwa na langu zimwi Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Mzee mpenda watu, hanioni mie kwani Nazimaliza sapatu, kumfata kikashani Kwake sisikiki katu, hanipi ‘ta tumaini Naitupa mishororo, bora nifanye muziki Yule mhindi wa pwani, makundini simuoni Hivi yuwapi jamani, Raneti aniauni Azitupe ‘ko hewani, nisikike redioni Naitupa mishororo, bora nifanye… Read more Umalenga ni basi.

Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?

Salamu ziloyakini, wajumbe tusikizeni, Tubebazo kwa makini, tunataka wajuzeni, Mengi tumeyabaini, nanyi tuwaulizeni, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Umma wawasubirini, toka huko mitaani Asilimia tisini, watetezi mu njiani, Vipi hamujiamini, na kujishusha thamani, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Enyi wasomi nchini, nawaeleza bayani, Tuikamateni dini, tuepuke ushetani, Hapo tutajaaini, na kujua kiundani, Kwamba wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Jamii inatamani, ile elimu auni, Kuondolewa gizani, kuepuka hali duni, Tusiwepo mashakani, mutupunguze huzuni, Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini? Jama! tuelimisheni, watu waache uhuni, Dhima… Read more Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?

Mwenye kupaka midomo.

Nauliza si utani,wala sizuwi fitina Naomba jibu wendani,lenye kina na maana Hii rangi midomoni,huwa ina ma’na gani? Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Mahaba mnatatiza,mabinti wa siku hizi Nyoyo mnatuumiza,kisi sasa hatuwezi Midomo mnashangaza,walahi mwatupa kazi Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Rangi hii midomoni,nyengine hasa ni sumu Haina raha jamani,mapenzi kukosa hamu Mwatunyanyasa wendani,kisha na kutudhulumu Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Majike mloolewa,lengo lenu huwa gani? Kikweli mwajiumbuwa,hamvutii jamani Na yule ulochumbiwa,kisi upigwaje hani? Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Dume fulani majuzi,lilisaka sidechiki Kapigwa kisi mjuzi,penzi na yake mikiki Kurudi nyumbani… Read more Mwenye kupaka midomo.

Rais Fungua nchi.

Kwa muda tumenyamaza,lakini tumerejea, Hata kama twajikaza,ni mengi tumepitia, Na nyumbani twajilaza,sadirini twaumia, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Korona imepungua,na sasa wangoja nini? Wananchi twashangaa,mikutano hadharani, Ninakusihi fungua,tusiumie mbeleni, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Twaona nazo siasa,wabunge watukanana, Hawaoni ni makosa,inafaa kuwakana, Hakuna wa kuwanasa,ukweli kuna korona? Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Kila siku twakereka,hatuna matumaini, Ukweli twalalaika,tukiwa huku nyumbani, Vipi tutasaidika,na shida hizi jamani? Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Mjini na vijijini,watoto wamepotea, Tuambie zako plani,za nchi kuifungua, Twangoja yako idhini,kwa muda ‘mevumilia, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Na… Read more Rais Fungua nchi.

Nani aliwaroga.

NANI AMEWAROGA? Lipokuja divolusheni, kadhani sluhu mepata, Usilojua Jamani, ni usiku wa matata, Kura liwapigieni, gavana na maseneta, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Meoza moja samaki, mtungo u mashakani, Wananchi wamehamaki, magavana chunguzeni, Mafisadi Kawasaki, pesa zetu okoeni, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Sonko kumi milioni, taachama kwa Korane, Mia mbili milioni, zi mfukoni mwa Korane, Wakifika kortini, dhamana si Mara nne , Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Ni makubwa ya Obado, ligawa na familiya, Mehukumiwa Obado, ila pesa mesaliya, Twalalamika si bado, pesa kuturudishiya, Hivi leo… Read more Nani aliwaroga.

Nani aliwaroga.

NANI AMEWAROGA? Lipokuja divolusheni, kadhani sluhu mepata, Usilojua Jamani, ni usiku wa matata, Kura liwapigieni, gavana na maseneta, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Meoza moja samaki, mtungo u mashakani, Wananchi wamehamaki, magavana chunguzeni, Mafisadi Kawasaki, pesa zetu okoeni, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Sonko kumi milioni, taachama kwa Korane, Mia mbili milioni, zi mfukoni mwa Korane, Wakifika kortini, dhamana si Mara nne , Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Ni makubwa ya Obado, ligawa na familiya, Mehukumiwa Obado, ila pesa mesaliya, Twalalamika si bado, pesa kuturudishiya, Hivi leo… Read more Nani aliwaroga.

Mashairi Bomba.

SHAIRI: KUMBE NI…… MTUNZI: FAM Sikuwa na wasiwasi, katika yangu safari, naeleza Sikutaka mfuwasi, wala sikupanda gari, sikiliza Sikupenda kujighasi, sikuifanya kikiri, sikuweza Nilikwenda polepole Njia nikaiandama, sio ya barabarani, nawambia Popote sikusimama, japo yekuwa mwituni, mwasikia Khofu kwangu ikahama, hatembea kwa amani, sehofia Sikuogopa chochote Kwa mbali nikasikia, sauti iliyo kali, inanita Huku kwato zanijia, zimekazana kwa kweli, sikusita Na wala sikukimbia, nikenda bila kujali, kwatakwata Njia nikaiandama Nilipofika kwa mbele, wallahi sikuamini, sikioni Nesikia makelele, yasema Mimi ni jini, maluuni, Metumwa nije nikule, kafara ya kijijini, huamini? Moyo… Read more Mashairi Bomba.

Mashairi yanayozuzua.

TUACHE MATAMANIKO. Karibuni nisongele, kaeni kwa mzunguko, Kigodani niketile, nitemele mzinduko, Wenye mvi linemele, tamaa ni maanguko, Tuache matamaniko, mauti situfikile. Umero jipu tumbule, huyaleta masumbuko, Utake hili na lile, hadi kufanya tambiko, Huoni wang’oka nywele, na hupati tuliziko? Tuache matamaniko, mauti situfikile. Kiwa mepata mawele, kubali ndiyo ya kwako, Mbona utake mchele, na sio kiwango chako? Rahimu nd’o mgawile, siletile chokochoko, Tuache matamaniko, mauti situfikile. Ukipata kitungule, shukuru kwa goti lako, Siwe mpiga kelele, wa kumtaka kiboko, Watakani kubwa wele, ya dunia mapitiko? Tuache matamaniko, mauti situfikile. Tamaa ikiwa… Read more Mashairi yanayozuzua.