Skip to content

Category: Lugha na Sarufi

Aina na mbinu za tafsiri.

Tafsiri ya neno kwa neno. Hii ni tafsiri ambayo mofimu na maneno hufasiriwa yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia maana zake za msingi bila kujali muktadha wala muundo wala utamaduni wa lugha lengwa. Mpangilio wa mofimu na maneno wa lugha chanzi haubadiliki,pia tafsiri hii hulenga tu kupata maana ya kimsingi au ya kamusi. Katika tafsiri hii matini iliyofasiriwa huandikwa chini ya matini ya lugha chanzi. Tafsiri sisisi. Tafsiri hii hutoa maana za kimsingi za maneno yakiwa pwekepweke kwa kuzingatia kanuni za kisarufi za lugha lengwa hususani sintaksia. Mbinu hii haizingatii muktadha wala… Read more Aina na mbinu za tafsiri.

Aina za Tafsiri.

Aina za tafsiri za tafsiri ni kama zifuatazo: Tafsiri ya fasihi Tafsiri ya riwaya Tafsiri ya tamthiliya Tafsiri ya ushairi Tofauti ya tafsiri za kifasihi na zisizo za kifasihi. Tafsiri za matini za kisayansi/kiufundi. Matini za kisayansi au za kiufundi ni zile matini zinazotumia msamiati maalum, mfano matini za tiba, uhandisi, elektroniki, sayansi ya kompyuta na sayansi nyinginezo. Tafsiri ya matini hizi haijiegemezi katika utamaduni wowote na hutofautiana na tafsiri nyingine kutokana na matumizi makubwa ya istilahi. Matini za kiufundi pia hutumia picha, grafu, michoro, vielelezo, takwimu n.k na huandikwa… Read more Aina za Tafsiri.

Uhusiano baina ya tafsiri na lugha.

Taaluma ya tafsiri ni taaluma kama taaluma nyingine ambazo haziwezi kujitegemea bila kuhusiana na taaluma nyingine. Kama mwili wa mwanadamu unavyofanyakazi ambapo viungo vyake vyote vinategemeana katika kukamilisha majukumu ya kuona, kutembea, kula, kulala, kuongea n.k. Taaluma hii ya tafsiri ina uhusiano mkubwa na taaluma nyingine kama: o Ukalimani Tafsiri ni uhawilishaji wa mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja hadi nyingine. Ukalimani ni uhawilishaji wa ujumbe au mawazo ulioko katika mazungumzo kutoka lugha moja hadi nyingine. o Isimu linganishi Isimu linganishi ni tawi la isimu linalofanya uchanganuzi wa lugha… Read more Uhusiano baina ya tafsiri na lugha.

Sajili Ya Simu.

Hii ni lugha inayotumiwa katika mazungumzo ya simu. Sifa za lugha ya simu Mazungumzo ya simu ni mafupi, hutumia sentensi fupi zenye muundo rahisi. Hoja hutajwa moja kwa moja bila maneno mengi kwani ili kudhibiti gharama ya simu Huwa na kukatizana kwa maneno kati ya wazugumzaji. Huwa ni mazungumzo baina ya watu wawili pekee; anayepiga na anayepokea. Hutumia istilahi maalum za lugha ya simu kama neno ‘hello’ Huchanganya ndimi (kutumia maneno yasiyo ya lugha nyinginezo) ili kuwasilisha ujumbe kwa upesi. Ni lugha ya kujibizana.