Njia za kubainisha wahusika.

Uchunguzi wa historia na maendeleo ya fasihi unadhihirishwa kuwa, wahusika wa kifasihi hubadilika kadri wakati unavyoendelea. Wahusika wanaopatikana katika kazi za kifasihi za miaka ya zamani wanatofautiana kwa kiasi kikubwa na wahusika wanaopatikana katika kazi za fasihi za miaka ya baadaye. Njogu na Chimerah (1999:40-44), wanarejelea wahusika wanaozungumziwa Mlacha na Madumulla (1991). Wamitila (2008: 382-392),Continue reading “Njia za kubainisha wahusika.”

Mbinu za kusawiri wahusika.

Kwa mujibu wa Wamitila (2002), mwandishi anaweza kutumia njia kadhaa na tofauti katika kuwasawiri wahusika wake. Msanii ana uhuru sio tu wa kuwatumia wahusika wa aina fulani, bali wa kuiteua namna ya kuwawasilisha wenyewe. Kama wasomi na wahakiki wa fasihi, tunategemea sifa kadhaa kuwaelewa wahusika hao: maumbile yao, mienendo na tabia zao, lugha zao, vionjoContinue reading “Mbinu za kusawiri wahusika.”

Shairi la Kizuri chavutia

KIZURI Kizuri kinavutia, moyoni hata ozini,Yeyote hujitakia, kwa vyovyote maishani,Waja wajitafutia,kazini au nyumbani,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Kizuri chang’ang’aniwa, masikini na tajiri,Popote chapiganiwa, jambo hili siyo siri,Wengi wachanganyikiwa, njiani wakisafiri,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Uwe hata ni mwalimu, uhodari ni gharamu,Ukakamavu dawamu, kujituma ni lazima,Lazima ujilazimu, kuiboresha huduma,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Awe ni mke wandani, wapo waContinue reading “Shairi la Kizuri chavutia”

Dhana za falsafa ya historia katika riwaya.

Falsafa ya historia inahusu utaratibu maalumu na wenye kuzingatia umakini wa hali ya juu unaoongoza tafakari juu ya sura anuwai za zama zilizopita na ufahamu wa mambo ya kale. Falsafa ya historia inatuwezesha kuelewa kwamba historia inajitokeza katika sura mbalimbali, kwani hakuna historia iliyo katika sura ya aina moja. Pia, inatuwezesha kufahamu kwamba kuna ufahamuContinue reading “Dhana za falsafa ya historia katika riwaya.”

Changamoto na ufumbuzi wa riwaya za Kiswahili.

Licha ya kuwepo kwa mazingira mwafaka ya riwaya ya Kiswahili kutumika kufundishia historia, tukiri kuwa kuna changamoto kadha wa kadha ambazo kwa namna yoyote zinapaswa kushughulikiwa ipasavyo ili kufanikisha kwa uhakika riwaya ya Kiswahili kutumika kufundishia historia. Changamoto hizi zinajadiliwa katika sehemu hii kama ifuatavyo: Mosi, uhaba wa kupatikana kwa riwaya zilizochapishwa kale. Hili niContinue reading “Changamoto na ufumbuzi wa riwaya za Kiswahili.”

Riwaya za Kihistoria.

Riwaya za kihistoria ni tanzu za kimasimulizi ambazo huunda na kuitengeneza historia kwa njia ya ubunifu. Ubunifu huu unajitokeza kupitia wahusika wa kubuni au wahusika halisi ambao wameinuliwa kidogo katika namna ya utendaji wao kuliko hali halisi. Pia, ubunifu huo unaweza kujitokeza kupitia utumiaji wa matukio halisi ya kihistoria lakini yakaongezewa na wahusika wa kubuniContinue reading “Riwaya za Kihistoria.”

Fasihi na Historia.

Pamoja na uhusiano huo wa muda mrefu, ni vema ikatambulika kwamba zimekuwepo harakati kadhaa za kutaka kuifuta kabisa historia hii ya uhusiano huo. Wataalamu wa pande hizi mbili, kila upande kwa malengo yake katika kipindi fulani cha wakati, walifanya majaribio kuondosha au kuufuta kabisa uhusiano huu. Kwa upande wa wanafasihi walisukumwa na haja ya kuionaContinue reading “Fasihi na Historia.”