Lugha na Sarufi
Aina Za Wadudu.
- Funza/Tekenya-Huyu ni mdudu anayefafana sana na kiroboto na ambaye hupenya ngozini na kutaga mayai.
- Nzige-Mdudu ambaye husafiri masafa marefu na ambaye huharibu mimea kwa wingi.
- Tandu-Mdudu mwenye miguu mingi na ambaye huuma na ana sumu.
- Nondo-Mdudu anayefanya na kipepeo na hupenda kuruka usiku.
- Mbu-Mdudu ambaye hufyonza damu na kuuma watu na ambaye huhusika katika uambukizaji wa ugonjwa wa malaria.
- Mbungo-Mdudu mkubwa kuliko nzi, hufyonza damu na huhusika katika uambukizaji wa maradhi ya malale.
- Kiroboto-Mdudu ambaye huishi mwilini mwa mbwa,paka na hata wanyama wengine.
- Nyenze-Mdudu ambaye hutoa sauti kali usiku na hufanana sana na panzi.
- Kupe-Mdudu ambaye huganda mwilini mwa wanyama na kufyonza damu yao.
- Nyigu-Mdudu mwenye kiuno chembamba, huuma na aliye katika jamii ya ya nzi na nyuki.
- Kipepeo-Mdudu mwenye mbawa za kupendeza na aliye kama nondo ila ni mkubwa.
- Kumbikumbi-Mdudu ambaye huonekana katika makundi hasa nyakati za mvua.
- Kerengende-Ndege mkubwa mwenye jamii ya nzi.
- Jongoo-Mdudu mwenye miguu mingi myekundu na mwili mweusi.
- Chungu-Mdudu mweusi, mwenye jamii ya mchwa.
- Chawa-Mdudu ambaye hupenda kuishi kwenye nywele chafu na kunyonya damu.