Lugha na Sarufi
Aina za vihusishi.
Vihusishi ni aina ya maneno yanayoonyesha uhusiano baina/kati ya neno moja na jingine.Kuna aina mbalimbali za vihusishi kulingana na utendakazi wao.Dhima za vihusishi ni kama zifuatazo.
- Hutumika kuonyesha uhusiano kiwakati.K.m Wanafunzi walienda darasani baada ya kusikiliza hotuba ya mwalimu mkuu.
- Hutumika kuonyesha uhusiano wa mahali.K.m Walitembea kando ya barabara.
- Hutumika kuonyesha uhusiano wa umilikaji.K.m Wageni waliokuja kwangu wameondoka.
- Hutumika uhusiano wa sababu.K.m Polisi walimkamata kwa ajili ya wizi.
- Hutumika kuonyesha uhusiano wa kulinganisha.K.m Yeye alipata alama ishirini zaidi ya mimi.
Kutokana na dhima za vihusishi tunapata aina zifuatazo za vihusishi.
- Vihusishi vya sababu
- Vihusishi vimilikishi
- Vihusishi vya kulinganisha
- Vihusishi vya kifaa/chombo/ala
- Vihusishi vya namna
- Vihusishi vya mahali
- Kihusishi ‘na’ cha mtenda