Lugha na Sarufi
Aina Za Ndege.
- Dudumizi/Shundi/Gude/Tipitipi-Huyu ni aina ya ndege asiyejenga kiota.
- Kanga-Huyu ni kuku wa porini aliye na madoadoa meupe.
- Kasuku-Ndege aliye na rangi nyingi za kupendeza na hodari wa kuiga.
- Kigotago-Ndege ambaye hupigapiga mti kwa mdomo ili kupata vidudu.
- Hondo-Ndege aliye katika jamii moja ya shundishundi aliye na maji ya kunde na hupaza sauti kwa kawaida yake.
- Chozi-Ndege mdogo aliye na rangi ya manjano.
- Chiriku-Ndege mdogo ambaye hupiga kelele nyingi sana.
- Keremkeremu-Ndege ambaye hupenda sana kula nyuki.
- Korongo-Ndege aliye na miguu mirefu na shingo ndefu.
- Kware-Ndege mdogo kuliko kuku aliye na miguu myekundu na na mwili hudhurungi.
- Mbuni-Huyu ni ndege anayekwenda kwa kasi na ambaye ni kubwa na hana uwezo wa kuruka.
- Mnandi-Ndege mkubwa mwenye shingo ndefu,miguu mifupi mithili ya bata, tumboni ana rangi nyeupe na hupenda kuishi majini kuwinda samaki.
- Minga-Ndege mwenye rangi kijani,miguu myekundu,hula nazi na hupatikana katika jamii ya tetere.
- Njiwa-Ndege ambaye hufugwa nyumbani na huwa katika jamii ya tetere.
- Sigi-Ni ndege mdogo aliye na manyoya meusi kichwani na rangi ya kijivu kifuani.
- Shakwe-Ndege wa pwani anayefafana na membe na anayependa kula samaki.
- Tetere-Ndege mdogo mwenye rangi ya kijivujivu,hufafana na njiwa.
- Yangeyange/Dandala-Ndege mweupe na ana kishungi.
- Tongo-Hili ni jina la jamii la ndege wadogo warukao katika makundi.
- Mumbi-Ndege mkubwa anayeaminika kuleta msiba kila mahali aendapo.
- Kirumbizi-Ndege mdogo mwenye mkia mrefu na ushungi, hupiga kelele alfajiri.
- Kunguru-Ndege mweusi ambaye mara nyingi huwa na doa jeupe shingoni.
- Kipanga-Ndege ambaye hula wanyama na ndege wadogowadogo.
- Batabukini-Huishi zaidi majini,ni sawa na bata.
- Bata-Ndege anayependa matope.Ni mkubwa wa kuku.