Harambee stars.

*HARAMBE STARS*

Ya mgambo imelia,katika letu taifa,
Timu’tu’ noshabikia, tayari kusaka sifa,
Tachuana na Zambia,hapo Kesho ndo arafa,
Mzalendo miye Isa,ushindi nawatakiya.

Mzalendo miye Isa, ushindi nawatakiya,
Ushinde si wetu hasa! Hili ‘wahakikishiya,
Kikosi ni cha kisasa,chenye juzi nawambiya,
Ajabu nayo ni kwamba, mashabiki watokuwa.

Ajabu nayo ni kwamba, mashabiki watokuwa,
Kushudia wetu simba,makucha yao wakitowa,
Kuparuza kwenye dimba,chipolopolo lopewa,
Runingani nitakwama,hata weye nikidhani.

Runingani nitakwama, hata weye nikidhani,
Saa kumi nitapima,jitafutia kochini,
Niwaone kina Juma,olunga wetu nchini,
Wafula hata mogaka,kipchoge wote wanjiku.

Wafula hata mogaka, kipchoge wote wanjiku,
Wenye kipaji cha soka,wasiwatwe hiyo siku,
‘kufunzi kimakinika,tasherekea usiku,
Mabao tele tajaza,huko mbele tutasonga.

Mabao tele tajaza, huko mbele tutasonga,
Wakaweze kujikaza,mikono tutawaunga,
Umoja nawahimiza,ndo tafanya kuwafunga,
‘metoka hivi kidogo,kwenda kulipa ‘go’ tivi.

(Elisha otoyi ndiye malenga)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s