Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?

Salamu ziloyakini, wajumbe tusikizeni,
Tubebazo kwa makini, tunataka wajuzeni,
Mengi tumeyabaini, nanyi tuwaulizeni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Umma wawasubirini, toka huko mitaani
Asilimia tisini, watetezi mu njiani,
Vipi hamujiamini, na kujishusha thamani,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Enyi wasomi nchini, nawaeleza bayani,
Tuikamateni dini, tuepuke ushetani,
Hapo tutajaaini, na kujua kiundani,
Kwamba wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jamii inatamani, ile elimu auni,
Kuondolewa gizani, kuepuka hali duni,
Tusiwepo mashakani, mutupunguze huzuni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jama! tuelimisheni, watu waache uhuni,
Dhima tuiepukeni, tusije kufanywa kuni,
Dini tulinganieni, yasije ya filauni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jamani jitambueni, muwapo kule Ndakini,
Eti Bweni kiumeni, dada anafata nini,
Au bweni la kikeni, dume lakaa kitini,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Kaditama ukingoni, nudhumu yangu mwishoni,
Wasomi toka vyuoni, kwetu ninyi ndio mboni,
Ujumbe pasi na soni, wa anuani tungoni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini

(Mtunzi: Abdallah Hanga)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s