Skip to content

Month: August 2020

Umuhimu wa Kiswahili.

Kitaifa: Katika kiwango cha kitaifa lugha ya Kiswahili kina majukumu yafuatayo:  Ni chombo cha mawasiliano katika kiwango cha kitaifa, Kikanda na kimataifa kama ilivyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika (UA).  Ni kitambulisho muhimu cha utaifa na uzalendo wetu.  Ni kitambulisho cha watu wa Afrika Mashariki. Kiswahili ni lugha ya taifa na vilevile lugha rasmi nchini Kenya na Tanzania.  Hutumika katika uandishi na uchapishaji. Vitabu vingi vimeaandikwa au kutafsiriwa kwa Kiswahili, kwa mfano Biblia Takatifu, Daftari la Isimujamii.  Ni kigezo cha kuchujia… Read more Umuhimu wa Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili kama msingi wa elimu.

Kiswahili kinatambulika kama lugha ya Afrika Mashariki. Kwa miaka mingi sasa imekuwa ikipata hadhi ya lugha ya Kimataifa, licha ya kwmba imekuwa ndio njia kuu ya mawasiliano baina ya watu wa makabila tofauti. Sifa hizi zote ni ushahidi wa haraka tu kwamba Kiswahili ni lugha ambayo imeweza kujenga misingi maalum ya maarifa ya wazungumzaji wake. Hii inatokana na kuwa hizi ni sifa zinazodhihirisha kuwa Kiswahili kinaweza kuzielezea dhana tofauti za watu wa aina mbalimbali na zikaeleweka kwa wazungumzaji wengine na hivyo watu kuelewana. Aidha kinaweza kuchukua dhana za kigeni na… Read more Lugha ya Kiswahili kama msingi wa elimu.

Utandawazishaji wa Kiswahili kupitia simu.

Mojawapo ya matokeo ya utandawazi ni kuwapo kwa simu za kiganjani1 na matumizi yake. Siku hizi nchini Tanzania mawasiliano ya simu yamekuwako kwa wingi kuliko ilivyokuwa tangu wakati wa uhuru hadi katikati ya miaka ya tisini. Mahali ambapo hakukuwa na mawasiliano kabisa, kama sehemu nyingi za vijiji vya Tanzania, siku hizi kuna mawasiliano kwa njia ya simu hizi za kiganjani na lugha inayotumika katika mawasiliano haya ni Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inayotumika katika simu hizi ni ya kiutandawazi na pengine si rahisi kuiona nje ya wigo huu wa kiutandawazi ambao… Read more Utandawazishaji wa Kiswahili kupitia simu.

Utandawazi na mawanda ya matumizi ya simu.

Utandawazi na Mawanda ya matumizi ya simu Jamii nyingi za Kitanzania kama zilivyo nyingi katika Afrika, bado zinaishi vijijini ambako hakuna umeme. Aidha katika vijiji kama hivyo, hakukuwa na mawasiliano ya ‘simu za mezani’. Kwahiyo, ilikuwa haiyumkiniki kuwa na mawasiliano kwa njia rahisi bila kuwepo kwa miundombinu hasa umeme na simu. Upatikanaji wa simu za viganjani, na kukua kwa matumizi yake kumeleta mabadiliko makubwa na kurahisisha mawasiliano. Matumizi ya simu hizi mijini na vijijini ni mojawapo ya matokeo chanya ya utandawazi. Simu hizi za viganjani zinatumika kwa wingi miongoni mwa… Read more Utandawazi na mawanda ya matumizi ya simu.