Skip to content

Month: July 2020

Sifa za lugha tandawazi.

Kimsingi, kuna sifa bainifu moja katika lugha tandawazi ambayo ni ‘ufupishaji’. Ufupishaji huu unatokea kutokana na ‘udondoshaji’, ‘unambaishaji’ na ‘umatamshi’. Sifa hizi ingawa zinaweza kuangaliwa kama zinazojitegemea, ni vijitawi tu vya sifa moja kuu yaani ufupishaji. Kama nitakavyoonesha hivi punde, lengo la sifa hizi tatu: ‘udondoshaji’, ‘unambaishaji’ na ‘umatamshi’ hulenga kufupisha neno, sentensi au kifungu cha sentensi ili mhusika aweze kutuma maneno mengi iwezekanavyo kwa kutumia nafasi ndogo. Kwa maneno mengine anafanya mawasiliano ‘marefu’ kwa kutumia maneno machache. Sifa hizi zimeelezwa kwa undani na wataalamu kama vile Crystal (2001, 2004,… Read more Sifa za lugha tandawazi.

Mabadiliko na Uchanganyaji msimbo katika Isimujamii.

Kwa mujibu wa Wanaisimujamii, kuna miundo miwili ya lugha katika Isimujamii. Moja ni muundo wa kubadili misimbo na wa pili ni muundo wa kuchanganya misimbo. Kwa mujibu wa Weinreich (1953), aliyenukiliwa Naseh (1997: 202), ubadilishaji misimbo hutokea katika mazingira ya mazungumzo pale “watu wenye zaidi ya lugha moja wanapobadili msimbo kutoka lugha moja kwenda nyingine kwa mujibu wa taratibu za mabadiliko katika lugha.” Naye Hymes (1974) anaeleza ubadilishaji msimbo kuwa ni matumizi ya lugha mbili au zaidi zinazogusa sentensi zaidi ya moja, au hata mitindo tofauti ya lugha. Ufafanuzi wa… Read more Mabadiliko na Uchanganyaji msimbo katika Isimujamii.

Dhana Ya Wahusika.

Dhana ya wahusika katika kazi za fasihi imewahi kufasiliwa na watafiti kadhaa. Kama ilivyokwishaelezwa kuwa wahusika katika kazi za fasihi ni viumbe wanaopatikana katika hadithi yoyote ile. Viumbe hawa huwa sehemu ya kazi nzima. Pili, wahusika ni binaadamu wanaopatikana katika kazi ya kifasihi, na ambao wana sifa za kimaadili, kitabia, kiitikadi, kifalsafa ambazo hutambulishwa na wanayoyasema na wanayoyatenda. Wahusika huweza kutambulishwa pia na maelezo ya mhusika au msimulizi, msingi wa hisia, hali ya kimaadili, mazungumzo na matendo ya wahusika ndio kiini cha motisha au uhamasishaji wa wahusika (Wamitila, 2002). TUKI… Read more Dhana Ya Wahusika.

Njia za kubainisha wahusika.

Uchunguzi wa historia na maendeleo ya fasihi unadhihirishwa kuwa, wahusika wa kifasihi hubadilika kadri wakati unavyoendelea. Wahusika wanaopatikana katika kazi za kifasihi za miaka ya zamani wanatofautiana kwa kiasi kikubwa na wahusika wanaopatikana katika kazi za fasihi za miaka ya baadaye. Njogu na Chimerah (1999:40-44), wanarejelea wahusika wanaozungumziwa Mlacha na Madumulla (1991). Wamitila (2008: 382-392), amegawanya wahusika katika makundi manne. Mhusika wa jadi, mhusika wa kimuundo au kimtindo, mhusika wa kihalisi na mhusika wa kisasa. Mhusika wa kijadi. Dhana ya kijadi inakwenda na suala la wakati na hasa wakati wa… Read more Njia za kubainisha wahusika.

Mbinu za kusawiri wahusika.

Kwa mujibu wa Wamitila (2002), mwandishi anaweza kutumia njia kadhaa na tofauti katika kuwasawiri wahusika wake. Msanii ana uhuru sio tu wa kuwatumia wahusika wa aina fulani, bali wa kuiteua namna ya kuwawasilisha wenyewe. Kama wasomi na wahakiki wa fasihi, tunategemea sifa kadhaa kuwaelewa wahusika hao: maumbile yao, mienendo na tabia zao, lugha zao, vionjo vyao, uhusiano wao na wahusika wengine, hisia zao kwao na wengine, mazingira na mandhari yao, kiwango chao cha elimu, jamii yao nakadhalika. Mbinu zinazotumika kusawiri wahusika ni kama vile; mbinu ya kimaelezi, mbinu ya kidrama,… Read more Mbinu za kusawiri wahusika.