Shairi la Kizuri chavutia

KIZURI

Kizuri kinavutia, moyoni hata ozini,
Yeyote hujitakia, kwa vyovyote maishani,
Waja wajitafutia,kazini au nyumbani,
Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri.

Kizuri chang’ang’aniwa, masikini na tajiri,
Popote chapiganiwa, jambo hili siyo siri,
Wengi wachanganyikiwa, njiani wakisafiri,
Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri.

Uwe hata ni mwalimu, uhodari ni gharamu,
Ukakamavu dawamu, kujituma ni lazima,
Lazima ujilazimu, kuiboresha huduma,
Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri.

Awe ni mke wandani, wapo wa kategoria,
Yule hodari jikoni, kisura na kitabia,
Popote hapatikani, ni adimu nawambia,
Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri.

Kizuri chataka muda, bidii pasi kukoma,
Namba wani jitihada, kwenye bonde na milima,
Kwenye raha hata shida, mazuri yataka wema,
Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri.

(Toney Francis Ondelo
“Chomsky Mswahili/ Malenga Mjalisiha)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s