Mashairi kuhusu Korona.

Navalia barakoa,sokoni mie niende.
Yeye aliyoifua,safii bila ya mende.
Nilikuwa ‘mevalia,alipoifua Sinde
Korona mharibifu,ni lini utaondoka?

Madukani nifikapo,mita mbili wa’nekana.
Madukani wakaapo, usoni zaonekana.
Watu wote waendapo, barokoa waziona.
Korona mharibifu, ni lini utaondoka?

Unawadia wakati, kafiu hili kuanza.
Waondolewa kwa viti, karibuni litaanza.
Naye kukalia siti,taka safari kianza.
Korona mharibifu,ni lini utaondoka?

Askari nao waja,bila hata kukawia.
Saa moja imekuja,wakati wa kuishia.
Wengi awa ni wateja,onekana kulegea.
Korona mharibifu, ni lini utaondoka?

Nyumbani mie nafika,runinga nafungulia.
Ninanyo yaona kaka,korona mewazidia.
Waonekana na shaka,korona inaenea.
Korona mharibifu, ni lini utaondoka?

Chozi lanitoka mimi,niandikapo shairi.
Hataa ha¹liungami,yanitoka tiritiri!
Uchungu onja ulimi,ninapo hili kariri.
Korona mharibifu,ni lini utaondoka?

Ninakuomba Jalali, korona isitupate.
Janga la uchina hili,liache kuwa na kite.
Yaende haya makali, yasiweze ‘nea kote.
Korona mharibifu,ni lini utaondoka?

(Mwalimu Bosire Daniel
Bosiredaniel12@gmail.com)

Published by botieno835

Am a student of kiswahili

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

EmmatheMadeupMom

Mindfulness. Mental Health. Motherhood.

Lead Me The Way

Inspiring. Encouraging. Empowering.

Dr. Eric Perry

Psychology to Motivate | Inspire | Uplift

TIMU MAFANIKIO

Japhet Simon

swahilimax

blogu hii inahusu mawanda mapana ya maswala ibuka katika lugha ya Kiswahili na fani zake. Kimsingi, swahilimax hushughulikia mchipuko wa mambo muhimu kwa utendeti , tafsiri za istilahi zinazotumika katika maisha ya kila siku kwenye vyombo vya habari, kanisani, nyumbani, sokoni na kwenye taasisi za elimu.

swahilimedia

Siasa,Michezo,Burudani,Udaku,Muziki na Video Mpya kwa Lugha ya kiswahili

ASHIKI WA KISWAHILI

Ashiki wa Kiswahili

Info - Kenya

Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda, Love, mapenzi, Afya, Mazoezi ya mwili, Pesa, Elimu, Christianity, Ukristo, Money, Sleep, Fitness, politics, Biashara,health, Kiswahili, lugha, english, Sheng, Nairobi, Dar el salaam

WordAds

High quality ads for WordPress

MBUKUZI

House of informations

kiswahiliashirafu

Uhondo wa lugha ya Kiswahili

Discover

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Atavist Magazine

Uhondo wa lugha ya Kiswahili

Longreads

The best longform stories on the web

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.

%d bloggers like this: