Shairi la Kizuri chavutia

KIZURI Kizuri kinavutia, moyoni hata ozini,Yeyote hujitakia, kwa vyovyote maishani,Waja wajitafutia,kazini au nyumbani,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Kizuri chang’ang’aniwa, masikini na tajiri,Popote chapiganiwa, jambo hili siyo siri,Wengi wachanganyikiwa, njiani wakisafiri,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Uwe hata ni mwalimu, uhodari ni gharamu,Ukakamavu dawamu, kujituma ni lazima,Lazima ujilazimu, kuiboresha huduma,Hakihitaji haraka, hiki kilichokizuri. Awe ni mke wandani, wapo waContinue reading “Shairi la Kizuri chavutia”

Dhana za falsafa ya historia katika riwaya.

Falsafa ya historia inahusu utaratibu maalumu na wenye kuzingatia umakini wa hali ya juu unaoongoza tafakari juu ya sura anuwai za zama zilizopita na ufahamu wa mambo ya kale. Falsafa ya historia inatuwezesha kuelewa kwamba historia inajitokeza katika sura mbalimbali, kwani hakuna historia iliyo katika sura ya aina moja. Pia, inatuwezesha kufahamu kwamba kuna ufahamuContinue reading “Dhana za falsafa ya historia katika riwaya.”

Changamoto na ufumbuzi wa riwaya za Kiswahili.

Licha ya kuwepo kwa mazingira mwafaka ya riwaya ya Kiswahili kutumika kufundishia historia, tukiri kuwa kuna changamoto kadha wa kadha ambazo kwa namna yoyote zinapaswa kushughulikiwa ipasavyo ili kufanikisha kwa uhakika riwaya ya Kiswahili kutumika kufundishia historia. Changamoto hizi zinajadiliwa katika sehemu hii kama ifuatavyo: Mosi, uhaba wa kupatikana kwa riwaya zilizochapishwa kale. Hili niContinue reading “Changamoto na ufumbuzi wa riwaya za Kiswahili.”

Riwaya za Kihistoria.

Riwaya za kihistoria ni tanzu za kimasimulizi ambazo huunda na kuitengeneza historia kwa njia ya ubunifu. Ubunifu huu unajitokeza kupitia wahusika wa kubuni au wahusika halisi ambao wameinuliwa kidogo katika namna ya utendaji wao kuliko hali halisi. Pia, ubunifu huo unaweza kujitokeza kupitia utumiaji wa matukio halisi ya kihistoria lakini yakaongezewa na wahusika wa kubuniContinue reading “Riwaya za Kihistoria.”

Fasihi na Historia.

Pamoja na uhusiano huo wa muda mrefu, ni vema ikatambulika kwamba zimekuwepo harakati kadhaa za kutaka kuifuta kabisa historia hii ya uhusiano huo. Wataalamu wa pande hizi mbili, kila upande kwa malengo yake katika kipindi fulani cha wakati, walifanya majaribio kuondosha au kuufuta kabisa uhusiano huu. Kwa upande wa wanafasihi walisukumwa na haja ya kuionaContinue reading “Fasihi na Historia.”

Mashairi ya Kiswahili.

………… MWALIMU NAANGAMIA ………. mwalimu ninalilia, machozi yatiririka Serikali saidia, mwalimu ninateseka Nani atanikwamua, majanga yameniteka Mwalimu naangamia, sina kazi wala mlo Mbona ninasahaulika, mwelekezi wa shuleni Bunge sijatambulika, wakiwepo kikaoni Wabunge mnanizika, ninaenda kaburini Mwalimu naangamia, sina kazi wala mlo Tufanyapo mtihani, mwalimu ninasifika Nizamapo taabuni, jamii inanizika Niende wapi jamani, nchi imenigeuka MwalimuContinue reading “Mashairi ya Kiswahili.”

Dhana ya silabi.

Jumanne, (2014) Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za lugha hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Feng Shengli, (2003) Silabi ni mpangilio wa fungu la sauti za kutamkwa. David Crystal, (2003) Silabi ni sauti moja au zaidi inayowakilisha kifungu kimoja cha sauti katika lugha. Massamba naContinue reading “Dhana ya silabi.”