Shairi la Sabilia.

*ALLAH *ONDOA *KORONA
Hili janga limesibu, sote tujikarantini
Enyi wetu matabibu, suluhisho vumbueni
Gonjwa hili la ajabu, tumulilie Manani
Allah ondoa korona, janga hili linatishaCOVID-19 watakani?, watutesa binadamu
Wafagia si utani, unaua lau sumu
Umevuruga amani, maisha sasa magumu
Ewe korona ondoka, makao yako kuzimuChimbuko lako Uchina, ‘meenea duniani
Watutesa sie mbona?, watutia taabani
Na hatia si hatuna, waja si tumekosani?
Mungu wetu turehemu, janga hili ni tishioJitwalie kieuzi, mikono yako safisha
Tuyaachie mapuzi, gonjwa hili linafisha
Bila Mungu hatuwezi, tuombeni tukikesha
Ewe korona ondoka, ‘situtie mashakaniMegeuka mtandavu, ewe gonjwa liso tiba
Tumeshika tu mashavu, ‘metuacha na msiba
Umetujia kwa nguvu, koo zetu umekaba
Mola ondoa korona, janga hili janga bovuTwavalia barakoa, kujikinga nawe nduli
Uhai wewe watoa, metujia kwa ukali
Mungu ataja t’okoa, yatupasa si tusali
Gonjwa hili litashindwa, Mungu wetu yuawezaMungu mwumba turehemu, janga hili t’ondolee
Twakuomba utukimu, kwa maovu tusamee
Twakuita kwa awamu, ukombozi tuletee
Ewe korona ondoka, makao yako kuzimuTuiombee dunia, korona mekuwa smbo
Hofu tele metutia, metunasa lau chambo
Ulimwengu unalia, hili janga ndio wimbo
Allah ondoa korona, ulimwegu ukomboe( Mtunzi: Mwalimu Ephrahim
Tuzidi kuomba kwa imani janga hili lisitufakamie. Dunia tambara bovu )

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s